Serikali
kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana
Shonza imesema Shirikisho la soka nchini TFF limesajiliwa chini ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano hivyo shughuli zake zote zipo chini ya
serikali.
Mh.
Shonza ameyasema hayo jana wakati akjibu swali la mbunge wa Singida
Mjini Mussa Ramashani Sima ambaye alihoji kuhusu mamlaka ya Waziri
katika kusimamia kazi za TFF ikiwemo mapato na matumizi ya shirikisho
hilo kutokana na katiba ya TFF kutoruhusu kuingiliwa na serikali.
''TFF
pamoja na viongozi wake wote, wanapaswa wanalazimika na hivyo
wanatambua mamlaka ya Waziri, kwasababu katiba ya TFF inatambua kuwa TFF
ni chombo cha mpira ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya Baraza la
Michezo ya 1967 na marekebisho yake ya mwaka 1971'', alisema Shonza.
Aidha
Mbunge Mussa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Singida
amemuomba Waziri kuhakikisha wanaibana TFF ili ipeleka mpango kazi
kwenye vyama vya mikoa ili kujua matumizi ya pesa za ruzuku zinazotolewa
kwa shirikisho hilo.
No comments:
Post a Comment