Baada
ya balozi wa Urusi huko Lebanon kusema kuwa majeshi ya Russia
yatatungua makombora yoyote yatakayo lenga Syria, Rais wa Marekani
Donald Trump amesema Jumatano kuwa Russia iwe tayari, “ kwani makombora
hayo yatapigwa nchini Syria,”
“Hamtakiwi
kuwa washirika wa Mnyama Anaeuwa kwa kutumia Gesi ya sumu wananchi wake
wenyewe na anafurahia!” Trump amesema hayo katika ujumbe wa Twitter
wakati Washington ikiendelea kupima namna ya kulishughulikia madai ya
shambulizi hilo la silaha za kemikali.
Urusi imesema makombora ya Marekani yanatakiwa kuwalenga “magaidi” na sio “serikali halali” ya Syria.
Msemaji
wa Kremlin Dmitry Peskov pia amesema Jumatano kuwa pande zote
zinazohusika katika mgogoro wa Syria wanatakiwa kujizuilia na vitendo
ambavyo vitalisambaratisha eneo hilo.
Saa
kadhaa baadae, Jeshi la Urusi lilisema kuwa litayaweka majeshi yake
huko Douma, eneo ambako shambulizi la kemikali linashukiwa kutokea
Jumamosi ambalo liliuwa watu wasiopungua 40. Urusi imesema majeshi yake
yataendelea kuhakikisha usalama wa mji huo.
Syria
imeeleza tishio la Marekani kwamba itashambulia kwa makombora kuwa ni
“shinikizo la kivita lisilo na maana,” shirika la habari la serikali ya
Syria limesema.
Umoja
wa Mataifa na washirika wake kadhaa wameelekeza lawama kwa majeshi ya
Syria kuwa yanahusika na mauaji hayo, wakati Syria na Urusi wamekanusha
kuwa majeshi ya Rais Bashar al-Assad yalihusika na shambulizi hilo la
kemikali.
Waziri
wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis amesema kuwa Marekani bado inafanya
tathmini ya kintelijensia juu ya shambulizi hilo lililotokea Syria.
“Tunakaa tayari kuchukua hatua za kijeshi mbalimbali iwapo zitakuwa
zinaafikiana na maamuzi ya rais,” amesema Jumatano.
No comments:
Post a Comment