Msanii wa bongo movies Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea
ameandika ujumbe mrefu kwa ajili ya kumpongeza Mh Paul Makonda baada ya
kuanzisha kampeni ya kusaidia wanawake ambao wametelekezwa na wanaume
zao na kuwaachia watoto kulea peke yao.
Thea aliandika hivi kuhusu kampeni hiyo ya Mh Paul:
"Kwanza
nimpogeze mheshimiwa paul makonda kwa kujitolea na kulikumbuka kundi
hili la wanawake waliojitokezwa, kwakweli tatizo hili ni kubwa sana na
kumuachia Mh Makonda peke yake haitwezekana kwa sababu tatizo sio kwa
dar peke yake bali ni Tanzania nzima.
"Niombe
wadau wa maendeleo ya wanawake tanznia kutafuta suluhu ambayo ni
endelevu kwa tatizo hili.upo ukatili unaotokea kama ajali lakini ukatili
huu mwingi kwa wanawak na wasichana utokana na umaskini.
"Wanawake
hawa waliojitokeza leo inamaanisha kuwa hawajaweza kumudu mahitaji ya
msingi, nitoe wito kwa wanawake na wadau wengine kumuunga mkono Mh Paul
Makonda ili kuweza pia kuwakwamua wanawake hawa kiuchumi.
"Tuwasaidie
wanawake hawa kuwa na uchumi imara kwa sababu sio wanaume wote
wanakataa kutoa matunzo kwa makusudi, wengine wamekuwa wakiyumba.
Hata
hivyo kutokana na kampeni hii kila mtu amekuwa na muonekano tofauti kwa
sababu wapo wanaosapoti na pia wapo wanaosema zoezi haliwezi kumaliza
tatizo.
No comments:
Post a Comment