Umoja
wa nchi 28 Barani Ulaya zimekutana kwa ajili ya kusaka msimamo wa
pamoja kuhusu kushambuliwa kwa Syria huku baadhi ya nchi zikihofia
msimamo utakaochukuliwa na Urusi ambayo ndiye msambazaji mkuu wa gesi
barani humo.
Umoja
huo wa Ulaya unataka kujaribu kuangalia jinsi ya kushughulikia mgogoro
wa kidiplomasia ulioibuka na Urusi kufuatia suala la kushambuliwa kwa
Syria.
Aidha,
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wanataka kuwa na
msimamo wa pamoja na hatimaye kuwa na mshikamano kufuatia mgawanyiko
uliojitokeza baada ya mashambulizi yaliyofanywa nchini Syria.
Baadhi
ya wanachama wa Umoja wa Ulaya wamepinga vikali kuchukuliwa kwa hatua
ya aina yeyote ambayo inaweza kusababisha mgogoro huo kuongezeka.
Hata
hivyo, Mkutano wa leo unatarajia kujadili jinsi ya kuishinikiza Urusi
kujaribu kuumaliza mgogoro wa Syria, ingawa hadi sasa nchi kadhaa za
Umoja wa Ulaya zimeshindwa kuzungumzia hatua ya kushambuliwa kwa Syria
kwa sababu ya wasiwasi kuhusu msimamo utakaotoka Urusi ambayo ni
miongoni mwa nchi muhimu inayosambaza gesi barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment