Wachunguzi
kutoka Shirika la kudhibiti silaha za sumu OCPW walioenda nchini Syria
wamenyimwa kibali cha kuingia katika mji wa Douma kuchunguza madai ya
shambulizi la silaha za kemikali mjini humo.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Shirika hilo la OCPW, Ahmet Uzumcu katika mkutano
wa hadhara, ambapo amesema kuwa wachunguzi hao wamekosa kibali cha
kuingia katika mji yalikofanyika mashambulizi hayo mjini Douma.
Amesema
kuwa Serikali ya Syria pamoja na Urusi wamewanyima nafasi wachunguzi
hao kuingia mjini humo kwa sababu za kiusalama, ambapo amesema kuwa
mpaka sasa bado hawajaweza kuhakikishiwa usalama wao na haijawekwa wazi
ni lini hasa hilo litakapofanyika.
Hata hivyo Urusi na Syria zimekanusha madai ya kuwanyima kibali cha kuingia na kufanya uchunguzi katika mji huo wa Douma.
Zimesema hali hali ya usalama itaimarika, wachunguzi hao wataruhusiwa kesho Jumatano
No comments:
Post a Comment