Naibu
waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, ajira na watu wenye ulemavu Mh.
Antony Mavunde amesema kuwa Serikali inatambua kuwa wahitimu wa Elimu ya
juu ni wengi kuliko mafasi za ajira.
Waziri
Mavunde ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Hadija
Ally Mbunge viti maalum (CCM) lililohoji serikali imepanua fursa kwa
kuongeza vyuo vikuu nchini, je ni kiasi gani mfuko wa vijana unaweza
kuwanufaisha walengwa ikizingatiwa kuwa tatizo la ajira ni hali halisi
inayowakabili vijana.
Mavunde
amesema “Nafasi za ajira zinazotengenezwa kwa mwaka zimekuwa ni chache
kuliko wingi wa vijana hivyo basi serikali imeanza kuwabadili mitazamo
kuwa sio wote wanaoweza kukaa maofisini bali wanaweza kutumia uwezo wao
na kujiajiri katika sekta za kilimo na shughuli nyingine halali
zinazoweza wapatia kipato”.
Waziri
mavunde ameongeza kuwa Mfuko wa Maendeleo ya vijana umeweza kufikia
vikundi 397 ambapo zaidi ya Bilioni nne zimekwisha tumika kuwezesha
vijana kiuchumi.
No comments:
Post a Comment