Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Onesmo Maluda,
amekamatwa na Jeshi la Polisi na kuswekwa ndani kwa tuhuma za ubadhirifu
wa Sh. milioni 35.
Agizo
la kukamatwa kwa mwenyekiti huo ambaye pia ni diwani wa Kata ya Choma,
lilitolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokuwa
akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Choma
hivi karibuni.
Aliagiza
kukamatwa kwa viongozi wote wanaotuhumiwa kwa upotevu wa Sh. milioni 35
zilizotolewa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya ununuzi wa
mashine ya kukoboa mpunga ya Kijiji cha Choma.
Majaliwa
alieleza kuwa mashine hiyo licha ya kununuliwa, ilifanya kazi kwa muda
mfupi sana ikaharibika, hali iliyoleta sintofahamu kwa wananchi kutokana
na baadhi ya viongozi kulalamikiwa kununua mashine mbovu.
Waziri Mkuu alisema licha ya kulalamikiwa kwa ubovu, hata matengenezo yalishindikana.
Akitoa
taarifa baada ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo, Mkuu wa Polisi wilayani
humo, Ally Mkalipa, alisema mwenyekiti huyo alikamatwa na kuunganishwa
na watuhumiwa wenzake wanane kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa fedha
hizo.
Alisema
polisi wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine akiwamo mkandarasi,
Sadick Hans, ambaye alitoroka baada ya kusikia anatafutwa.



No comments:
Post a Comment