Benki
ya Wanawake (TWB) imeungana na Benki ya TPB baada ya benki hiyo
kushindwa kutimiza masharti ya kuwa na mtaji wa kutosha kujiendesha.
Kutokana na hatua hiyo, wateja, wafanyakazi, mali na madeni yote ya TWB yataunganishwa na Benki ya TPB kuanzia leo.
Hayo
yamesemwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens
Luoga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Alhamisi Agosti 2, kuhusu hatua mbalimbali benki hiyo ilizochukua kwa
baadhi ya benki ambazo zimekiuka masharti ya Sheria ya mabenki na
taasisi za fedha.
Amesema
Januari 4, mwaka huu iliziongezea muda wa miezi sita benki nne za
Tandahimba Community Bank (Tacoba), Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) na
Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) hadi Juni 30, mwaka huu ili
kufanikisha kiwango cha mtaji kinachohitajika na sheria za mabenki na
kanuni zake cha kiwango cha chini cha mtaji wa Sh bilioni mbili kwa
benki.
Aidha,
amesema hata baada ya muda huo kuisha na kuongezewa mwezi mmoja hadi
Julai 31, mwaka huu ili kukamilisha benki mtaji, benki mbili
zilifanikiwa huku TWB ikishindwa.
Ameanisha
Benki ya Tacoba na KCBL kwa sasa zimeongeza mtaji na kukidhi kiwango
knachohitajika kisheria na zitendelea na shughuli zake kwa mujibu wa
sheria kama kawaida.
“Kutokana
na hali hiyo, Wanahisa wa TWB na TPB Bank PLC, wameamua kuunganisha
benki hizo ili kuboresha ufanisi na utendaji wa benki hizo, hivyo
kutokana na muungano huo kutakuwa na benki moja ambayo itaendelea kuitwa
benki ya TPB Bank PLC.
“Benki
Kuu imeridhia uuganishaji wa benki hizo kuanzia Agosti 3, mwaka huu
ambapo itaendelea kuwa na mtaji wa kutosha kama sheria ya mabenki
inayotaka.
“Hivyo
wateja, wafanyakazi, mali na madeni yote ya TWB yataunganishwa na TPB,
muungano huo utaifanya muungano mpya kuwa imara zaidi na kuwa na mtaji
wa kutosha kama inavyotakiwa kisheria, chini ya kifungu cha 17, cha
sheria ya mabenki na taasisi za kifedha ya mwaka 2006.
“BoT inawaomba wateja wa TWB kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mpito cha uunganishaji wa benki hizi,” amesema Profesa Luoga.



No comments:
Post a Comment