Mbunge
wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bob Wine amekamatwa
muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki
haramu wa silaha nchini humo.
Muda
mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa
kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu
mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.
Mbunge
huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bob Wine leo
aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa
Uganda.
Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.
Mawakili
wa jeshi wameeleza mahakama kuwa mashtaka dhidi ya Wine yameondolewa na
kwamba mwanasiasa huyo akabidhiwe kwa polisi ili akabiliwe na mashtaka
ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa .
Wakili
wake Wine Medard Segona ameiambia mahakama kwamba licha ya kuwa
wameridhishwa na hatua ya mahakama ya kijeshi , anapinga hatua ya sasa
ya mteja wake kuhamishwa katika mahakama ya kiraia kukabiliwa na
mashtaka mapya.
Alitaka mbunge huyo aachiwe huru ili aweze kupelekwa kupokea matibabu.
Mahakama iliamua kuwa Bobi Wine yu huru, iwapo hakuna mashtaka mengine yatakayowasilishwa dhidi yake.
Wakati
huo Wine alionekana akilia na kupangusa machozi huku hukumu hiyo
ikisomwa. Alitoka nje ya mahakama akiwa anatemba kwa magongo na
kuonekana kuwa na maumivu makali. Hapo ndipo alipokamatwa upya.
Credit:BBC



No comments:
Post a Comment