Miongoni
mwa watuhumiwa hao ni mhandisi mshauri wa kampuni ya Y&P
Architects, Benjamin Kasiga ambaye anadaiwa kutoa taarifa ya uongo kwa
waziri huyo kuhusu ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji mkoani humo.
Tukio
hilo limetokea leo asubuhi Agosti 27, 2018 wakati Lugola na katibu mkuu
wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu walipofika katika kituo hicho
kwa kushtukiza.
Lugola
alipokuwa anakwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es
Salaam, alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku
akamatwe awekwe mahabusu kama polisi walitekeleza agizo lake.
Hata
hivyo, Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo akiwa chumba cha upelelezi badala
ya kuwekwa mahabusu ya polisi, hivyo akamuuliza kamanda wa polisi wa
mkoa huo, Lucas Mkondya sababu za kutotekelezwa agizo lake.
“Hivi
ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndiyo madudu mnayoyafanya? Tabia hii
siku zote tunaipinga ikichafua Polisi na hii ndiyo tabia yenu. Najua
ndiyo mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi,” alihoji Lugola.
“RPC
hawa polisi wako wanafanya nini? OCS njoo hapa, kwa nini umeweka hawa
watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani
kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi
huyu,” aliamuru Lugola.
Hata hivyo, Mkondya alimweleza Lugola kuwa polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.
Naye
mkuu wa kituo hicho, Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale
watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, amesema sababu kubwa ya
kutowaweka mahabusu ni kwamba chumba kilijaa na wanafanya hivyo mara
chache inapotokea.
Lugola aliipinga kauli hiyo kuhusu mahabusu hiyo kujaa wakati nafasi ya kukaa watuhumiwa hao ilikuwapo ndani ya mahabusu hiyo.





No comments:
Post a Comment