Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Godfrey Mwambe amewataka
viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa na
mawaziri kuacha kutoa matamko na maagizo kwa wawekezaji nchini.
Amesema
ni vema kila mamlaka ikatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na
kufafania iwapo kuna tatizo lolote likiwemo la kodi,vibali au bora wa
bidhaa kwa muwekezaji yoyote haja ya kufuata taratibu za kutafuta
ufumbuzi kupitia mamlaka husika badala ya kutolewa maagizo ambayo
hazingatii sheria.
Mwambe
amesema hayo leo jijini Dar es Saalam wakati anazungumzia ziara ambayo
TIC pamoja na wadau wanaohusika na sekta ya dawa na vifaa tiba nchini
ambayo waliifanya Korea Kusini na China, tuzo waliyoipata ya kushika
nafasi ya pili katika Maonesho ya Nanenane pamoja na kueleza majukumu
yao ya kuelimisha umma na kumasisha uwekezaji.
Hivyo
ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuna wimbi la viongozi kutoa maagizo
na matamko na hasa yanayohusiana na masuala ya kikodi,vibali na mambo
mengine.
Amesema
kwamba TIC wanafanya kazi kubwa na ngumu ya kuhamasisha wawekezaji na
mitaji kuja nchini na wanatumia gharama katika kufanikisha
“Kama
kuna muwekezaji yoyote ana tatizo lolote wa kufahamishwa na ni kituo
cha wawekezaji.Ni jambo la kushangaza Mkuu wa Wilaya anatoa makadirio ya
kodi, anatoa siku mbili kodi ilipwe wakati sheria haiko hivyo.
”
Unapozungumzia suala la kodi kuna utaratibu wake na sheria zake,hivyo
iwapo kuna tatizo la kikodi kwa muwekezaji kiongozi wasiliana na mamlaka
husika watatafuta ufumbuzi wake.
“Kama
ni suala la vibali wapo wanaohusika na vibali kwa ajili ya
wawekezaji,hivyo fuata utaratibu badala ya kutoa maagizo wakati huna
mamlaka ya kufanya hivyo,” amesema.
Ameongeza
kwamba viongozi wote jukumu lao ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika na
si kutoa maagizo na miongozo bila kufuata taratibu.
Amefafanua
kuwa TRA wapo vizuri katika kufanya shughuli zao na wanacho kitengo cha
uchunguzi hivyo kama mkuu wa wilaya au waziri unahisi kodi inayolipwa
na muwekezaji ni ndogo au hajalipa muda mrefu lazima utaratibu ufuatwe.
Ametoa
mwito kwa viongozi wote kushirikiana na TIC katika kuhakikisha
wanaendelea kuweka uaminifu kwa wawekezaji ili kifikia uchumi wakati.
Pia
ameomba ngazi zote za kimamlaka kila mmoja kusimama katika mipaka yake
kwani kila mmoja yupo kisheria na sababu za kueleza hayo ni kukumbusha
wajibu wa kila taasisi kutekeleza majukumu yake bila kuingia mipaka ya
mwingine.
Mwambe
ameeleza pia atamuandikia barua Kamisha wa TRA kumueleza umuhimu wa
maofisa wake wa kodi kukusanya kodi kwa wawekezaji badala ya kumuacha
muwekezaji anakaa miaka saba bila kulipa kodi.
“Kuna
taarifa ya hivi karibuni muwekezaji amekaa miaka saba hakudaiwa
kodi,anakuja mwingine mpya ndio anadaiwa na ile kodi ya miaka ya
nyuma.Huu ni uzembe.
“Kwanini
miaka yote ofisa wa TRA hawezi kwenda kukusanya kodi?Huo ni uzembe,
nitahakikisha nasimamia hili kwa kuzungumza na Kamishna wa kodi,”
amefafanua.Mwambe na kusisitiza lazima TRA wakusanye kodi.
Kuhusu
ziara ya Korea Kusini na China,amesema Agosti 10 had I 18 mwaka hui
aliongoza ujumbe wa wadau wanaohusika na dawa na vifaa tiba wakiwamo
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)pamoja na Chama cha wenye viwanda vya
dawa za binadamu na vifaa tiba.
Mwambe
amesema Agosti 13 wakiwa Korea Kusini walifanya kongamano ambalo
lilihusisha zaidi ya kampuni 100 wanaohusika kwenye eneo na pia
wanafanya kongamano China.
Amesema
matokeo ya ziara hiyo kuna kampuni tano ambazo zinahusika na uzalishaji
dawa na vifaa tiba watakuja nchini Septemba mwaka huu kwa ajili ya
mazungumzo kwani wanataka kuwekeza hapa nchini.
“Kampuni
zote ambazo zilishiriki wanatambuliwa na HWO na kwamba ushawishi mkubwa
ulikuwa kuwahamasisha waje kufanya uzalishaji dawa na vifaa tiba
nchini,” amesema.
Amesema
kikubwa ambacho TIC inatamani kuona ni uwekezaji wenye tija ambazo
utatoa fursa Watanzania kunufaika na kuchangamkia fursa zilizopo.
Akizungumzia
ushiriki wa maonesho ya Nane nane na kwamba wanazokanda saba katika
kuboresha utoaji huduma kwa wadau na lengo lao Kubwa ni kutoa elimu kwa
watanzania.
Amesema
wamefanikiwa kushika nafasi ya pili katika ubora wa utoaji huduma na
hasa katika kuwafikia wananchi na katika maonesho hayo waliwatembelea
wajasiriamali waliokuwa kwenye mabanda mbalimbali kutoa elimu.
Kuhusu
utendaji kazi wa pamoja ambapo TIC kuna kitengo maalum ambacho
kinahusisha taasisi mbalimbali kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma
kwa wawekezaji kwa haraka.
Amesema
kutokana na uwepo wa kitengo hicho wamekubaliana na NIDA nao wawepo
ndani ya kituo hicho na tayari maofisa wawili wa NIDA wamewasili hapo.
Hivyo
amesema wawekezaji wote wanaohitaji vibali vya NIDA watavipata TIC.Pia
ameelezea umuhimu wa kuwawezesha wajasiriamali waliopo nchini kwani ndio
muhimili wa maendeleo ya nchi.
Amesema
nchi nyingi ambazo zimefanikiwa ni kwasababu ya wajasiriamali na kwamba
TIC wanataka kuona wajasiriamali wanashiriki katika shughuli mbalimbali
baada ya wawekezaji kuingia.
Amefafanua
kwa mtazamo wake haoni sababu ya Dangote kuingiza magari 600 kwa ajili
ya kubeba saruji, kwani hilo lilipaswa kufanywa na watanzania.
Ameongeza haiwezekani Dangote ahangaike kuzalisha saruji na wakati huo huo anahangaika na kusafirisha saruji.
Amesema jukumu muwekezaji baada ya kuzalisha kazi inayofuata ni watanzania kuchangia fursa hizo.
“Watanzania waamke na waone kuna fursa nyingi ambazo wakizitumia vizuri zitasaidia kuendeleza shughuli za kiuchumi,” amesema.
Pia
amesema jukumu lao TIC ni kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali ikiwa
pamoja na kuwajengea uwezo na kuwaunganisha na na lengo ni
kuwaunganisha na kampuni kubwa.
“Malengo ya Rais ni kuona Watanzania wanafanikiwa na ndicho ambacho hata TIC nasi tunakisimamia,” amesema.



No comments:
Post a Comment