Mahakama
ya Wilaya ya Iringa leo inatarajia kutoa mwongozo wa kesi ya
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kama
atakuwa na kesi ya kujibu au la baada ya upande wa mashitaka kuhitimisha
ushahidi wao.
Nondo
anakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kuchapisha taarifa za uongo
mtandaoni Machi 7, mwaka huu akiwa eneo la Ubungo, Dar es Salaam na
kuzisambaza kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwamba yupo hatarini.
Katika
shtaka la pili, anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma
Mafinga alipokuwa anatoa taarifa kwa askari kwenye Kituo cha Polisi
Mafinga kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana Dar es Salaam na
kupelekwa Kiwanda cha Pareto Mafinga.
Katika
kesi hiyo Nondo anatetewa na mawakili wawili wakiongozwa na Jebra
Kambole chini ya mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC).



No comments:
Post a Comment