Mwenyekiti
wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo anayekabiliwa na mashtaka
ya kusambaza taarifa za uongo akidai kutekwa amekutwa na kesi ya kujibu.
Uamuzi
huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 27, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Mkoa wa Iringa, Liad Chamshama baada kupitia ushahidi wa upande wa
mashtaka.
Hakimu
Chamshama amesema kutokana na uamuzi huo, Nondo anatakiwa kujitetea
dhidi ya mashtaka yanayomkabili ambapo anatakiwa kujitetea.
Nondo
anatarajia kuleta mahakamani mashahidi wasiopungua watano kutoa
ushahidi katika kesi yake hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa kati ya
Septemba 18 na 19, mwaka huu.
Nondo
ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), kabla hajasimamishwa masomo kutokan ana kesi hii,
anadaiwa kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar es Salaam kuwa
ametekwa na shtaka la pili anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa polisi
katika Kituo cha Mafinga mjini Iringa.



No comments:
Post a Comment