Mbunge
wa Kibakwe(CCM), George Simbachawene amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Bajeti huku akiahidi kuongoza kamati hiyo kwa
kuzingatia sheria na taratibu zilizopo kwa maslahi ya Taifa.
Simbachawene amechaguliwa jana kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Hawa Ghasia kujiuzulu.
Aidha
Mbunge wa Maswa Mashariki (CCM)Mashimba Ndaki naye amechukua nafasi ya
Makamu Mwenyekiti iliyoachwa na Jitu Son ambaye pia alijiuzulu.
Akizungumzia
kuchaguliwa kwake, Simbachawene amesema jana aliteuliwa na Spika wa
Bunge Job Ndugai kuwa mjumbe wa kamati hiyo baada ya kuhamishwa kutoka
Kamati ya Katiba na Sheria.
“Nilipofika
kamati ya Bajeti nikaambiwa Mwenyekiti na Makamu wake wamejiuzulu basi
nikapata Interest ngoja nigombee na wajumbe wamenipitisha kwa kauli
moja nataka niseme tu kwamba kamati ile nafahamu ni kamati muhimu katika
mhimili wa bunge na serikali,”amesema.
Amesema
misingi ya uendeshaji wake ipo kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria
hivyo atasimamia sheria zote zinazosimamia sheria.
“Pia tutafanya majukumu yetu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo lakini pia kwa maslahi ya Taifa,”amesema.
Mwenyekiti
huyo amesema haoni kama ni mzigo mkubwa sana kwake kwa kuwa anachojua
kazi yake ni kukusanya mawazo ya wajumbe ili kutoa ushauri kwa sababu
kazi ya Bunge ni kutoa ushauri kwa serikali.



No comments:
Post a Comment