Polisi
mkoani Kagera inamshikilia mwalimu Respicius Patrick wa shule ya msingi
Kibeta akituhumiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa darasa la tano,
Siperius Eradius.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi alisema kifo cha mwanafunzi huyo kilitokea jana akipelekwa hospitali.
Alisema
Patrick (50), ambaye ni mwalimu wa nidhamu anadaiwa kumpiga mwanafunzi
huyo akihusishwa na upotevu wa mkoba wa mwalimu Herieth Gerard (46)
uliokuwa na Sh75,000 na vitambulisho vyake.
Hata
hivyo taarifa kutoka eneo la tukio na kwa baadhi wa wanafunzi wa shule
hiyo, wakati mwanafunzi huyo akiendelea kuadhibiwa, pochi ikiyodaiwa
kuibwa ilipelekwa shuleni hapo na mwendesha pikipiki aliyemsafirisha
mwalimu Herieth wakati akienda kazini, akidai aliisahau.
Baba
wa mwanafunzi huyo, Justus Balilemwa alisema alimchukua mtoto huyo
kituo cha watoto yatima cha Ntoma baada ya mama yake kufariki dunia
akijifungua.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya rufaa Mkoa wa Kagera, Dk John Mwombeki alisema
uchunguzi wa awali wa mwili wa mwanafunzi huyo unaonyesha alama
zinazohusishwa na kupigwa.



No comments:
Post a Comment