Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amezungumza na kutaja chanzo
cha kifo cha marehemu, Mtawa Bartholomew aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha
na Mipango katika hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), kilichotokea jana
asubuhii mara baada ya mtawa huyo kujirusha kutoka ghorofani ya tano.
Mtawa
huyo aliamua kujiuua kutokana na kesi inayomkabili ya upotevu wa fedha
kiasi cha shilingi milioni 380 zilizobainika kupotea.
“Hadi
sasa tunaweza kusema kifo chake kimetokana na tukio la upotevu wa fedha
katika ofisi yake, akiwa kama mkuu wa kitengo cha fedha tulimkamata na
kumhoji kwa siku kadhaa kuhusiana na upotevu huo wa fedha na kumuachia
kwa dhamana, hivyo wakati akijirusha kujiua alikuwa nje kwa dhamana,”
amefafanua.
Kamanda
Shana amesema siku chache kabla ya kifo chake mtawa huyo alikamatwa na
kuhojiwa pamoja na watumishi wengine nane ambao walikuwa wakikabiliwa na
tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh milioni 380 za hospitali
hiyo.



No comments:
Post a Comment