Kuna
taarifa kuwa msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Mr. Nice amekwama Kampala
Uganda baaada ya promota Abtex wa Abtex Promotion kushindwa kumlipa
fedha msanii huyo ambaye walikubaliana kuwa angetumbuiza kwenye tamasha
la Ekyeppukulu, June 24, 2018 kwenye uwanja wa Namboole
Kutoka wakati huo (mwezi Juni) kumekuwa na uvumi kuwa Mr. Nice amekwama Kampala baada ya Abtex kushindwa kumlipa fedha zake.
Taarifa
zinaeleza kuwa Mr. Nice alifikia kwenye hotel Sport View ndani ya
Kirenga ambapo alikaa hapo kwa siku kadhaa kwa ajili ya tamasha hilo,
hata hivyo taarifa nyingine zinadai kuwa muimbaji huyo kabaki Kampala
kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.
Hata hivyo pia katika video iliyowafikia Mseto East Africa, Mr. Nice alijibu yote yanayozungumzwa kuhusu yeye kukwama Kampala.
"Kuna
uvumi kwamba Mr. Nice amekwama Kampala, ninaweza kukwama kwenye eneo
langu? Abtex hakunilipa hata asilimia moja. Huyu jamaa alipotea kabisa
na nilipata mateso lakini Mr. Nice ni jina kubwa hivyo nikajitenga
kwenye hali hiyo mwenyewe, haikuwa vizuri kwa wao kunifanyia hivi"
amesema.
Ili
kuthibitisha zaidi kwamba wanaomkosoa/kumbeza kuhusu hilo hawapo
sahihi, Mr. Nice alionyesha gari aina Range Rover 2018 ambayo anaendesha
kila siku akifurahia maisha Uganda huku bado akiendelea kuishi kwenye
Hotel.



No comments:
Post a Comment