Mnada
wa pili wa makontena 20 yenye samani zikiwamo meza na viti,
yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,
utafanyika Septemba Mosi baada ya ule wa Agosti 25 kutofanikiwa kupata
wanunuzi.
Makontena hayo ambayo yamekwama bandarini yanadaiwa kodi ya Sh bilioni 1.2.
Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa (TRA), Richard Kayombo, amesema
mamlaka hiyo imeazimia kufanya mnada wa pili Jumamosi ya wiki hii.
Alisema
mnada huo utaanza saa 2:00 asubuhi kwa kufuata taratibu zote za sheria
kama mnada wa awali ulivyofanyika, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza
kwa ajili ya kununua samani hizo kwa kufuata taratibu na sheria za
minada.
Alisema
TRA haiwezi kutangaza bei ya mnada huo kabla ya kufanyika kwa sababu ni
siri, lakini wateja watakaofika watakuta bei ambayo imepangwa kwa
mujibu wa sheria serikali iweze kupata mapato yake.
Aliwaomba wananchi kuondoa hofu kuhusu samani hizo na kuwataka kujitokeza waweze kununua samani hizo.
Baada
ya mnada wa Agosti 25 kukwama kwa wateja kushindwa kufikia bei
iliyotangazwa, Makonda alijitokeza na kusema mtu atakayenunua makontena
hayo aliyosema yana samani za shule za Dar es Salaam, atalaaniwa na
Mungu.
Baada
ya kauli hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alimjibu
Makonda akisema makontena hayo yatapigwa mnada mteja atakapopatikana
na wala hatishiki na laana zozote.



No comments:
Post a Comment