Jeshi
la Polisi mkoani Ruvuma limesema litaomba vyombo vya kutunga sheria
kuondoa biashara ya bodaboda, kufuatia madereva wa vyombo hivyo kutotii
magizo mbalimbali ya serikali ikiwemo la kuwataka kila mwendesha
bodaboda kuwa na kofia ngumu mbili.
Kauli
hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy
kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme alilolitoa
mwezi mmoja na nusu uliopita wa kuwataka madereva wa bodaboda
kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanakuwa na kofia ngumu mbili, jambo
ambalo bodaboda wanaonekana wameshindwa kulitekeleza huku wakitoa
sababu mbalimbali.
Mbali
na Kamanda huyo kusema hivyo nao baadhi ya abiria wa bodaboda mkoani
humo wamesema, hata wao wangependa kuvaa kofia hizo lakini linapofika
suala la kudai kofia, madereva bodaboda hao hutoa sababu zisizo na
msingi.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma amesema wamechukua hatua mbalimbali za
kuwakamata baadhi ya madereva bodaboda kuwaweka ndani na kuwafikisha
mahakamani lakini bado wamekuwa wagumu kutii bila shuruti.



No comments:
Post a Comment