Viongozi
wa zamani wa Chama Cha Ushirika Kagera (KCU 1990 Limited) wataendelea
kusota rumande baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoa wa Kagera
kuwanyima dhamana kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi
kwa ubadhilifu wa shilingi Milioni 218 wanaodaiwa kuufanya.
Akisoma
uamuzi kuhusu ombi la washitakiwa kutaka wapatiwe dhamana jana Agosti
27, 2018 hakimu mkazi mfawidhi, John Kapokolo alisema mahakama hiyo
haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi na kutaka maombi yao
yapelekwe kwenye mahakama sahihi.
Akizungumza
mara baada Hakimu Kapokoro kutoa uamuzi huo, mwendesha mashaka wa
serikali alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa
watuhumiwa hao kwa kuwa baadhi ya tuhuma zinazowakabili zinahusiana
masuala ya kuhujumu uchumi.
Kufuatia
uamuzi huo wakili anayewatetea watuhumiwa hao, Aron Kabunga alisema
mahakama hiyo haikuwatendea haki wateja wake kwani mahakama hiyo
haikuwa na sababu zozote za kuwanyima dhamana hadi kesi hiyo itapotajwa
tena Septemba 10, mwaka huu.
Washitakiwa
hao John Binunshu aliyekuwa mwenyekiti wa bodi, Vedastus Ngaiza
aliyekuwa meneja mkuu na Bestina Rwebangira walifikishwa katika mahakama
hiyo wiki iliyopita na kusomewa mashitaka matano.
Mashtaka yaliyosomwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Athumani Matuma ni kula njama, matumizi mabaya ya ofisi, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi nyaraka na kuhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh124 milioni.
Wakili wa washitakiwa Aaron Kabunga alipinga hati ya mashitaka kuwa iliunganisha makosa ya uhujumu uchumi na mengine bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa mashitaka na hivyo alitaka hati hiyo itupiliwe mbali na wateja wake wapewe dhamana.

Tayari
Serikali Ilishavunja Uongozi huu uliofikishwa mahakamani na kuchagua
uongozi mpya unaokiendesha chama hicho cha Ushirika KCU 1990 Ltd.

No comments:
Post a Comment