Jeshi
la Polisi jana lilivunja mkutano ulioandaliwa na taasisi za vijana
kuzungumzia mwenendo mbovu wa haki za binadamu na uvunjwahji wa haki za
msingi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkutano huo uliotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Landmark, Ubungo kuanzia saa tano asubuhi jana, ulikwama kuendelea baada ya kuvamiwa na polisi huku waandaaji wakitimua mbio kwa hofu ya kutiwa nguvuni.
Wakati
waandaaji wa mkutano uliopangwa kuanza saa tano asubuhi jana Agosti
26, 2018 katika Hoteli ya Landmark, Ubungo jijini Dar es Salaam
wakiendelea na maandalizi, ghafla aliingia ofisa mmoja wa polisi aliyekuwa amevalia sareza jeshi hilo na kujitambulisha kwa mlinzi kwamba naye ni mshiriki.
Baada
ya kupewa maelezo, ofisa huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana
alimweleza mlinzi huyo kuwa hawezi kuingia kutokana na sare zake za kazi
na kuita askari wengine waliovalia kiraia ambapo alitoka nje na baada
ya muda waliingia askari polisi waliokuwa na silaha za moto kwenye
ukumbi wa mkutano.
Hatua
hiyo ilizua taharuki miongoni mwa wanahabari na waandaaji wa mkutano
huo, baada ya kubaini kuzingirwa na askari kanzu waliovaa kiraia huku
askari wenye silaha wakizingira pia eneo hilo na hivyo kuwalazimu
waandaaji na wanahabari kila mmoja kuanza kutawanyika ki vyake.
Akizungumzia
tukio hilo, Mratibu wa Uhusiano kwa Umma wa Taasisi ya Tanzania Sahrawi
Solidarity Committee (TASSC), Noel Shao alisema walilazimika kusitisha
kutoa tamko lao ukumbini hapo baada ya kuhofia usalama kutokana na
kuzingirwa na polisi.
“Polisi
wenye sare na silaha na askari kanzu wakiwa ndani ya gari zisizo pungua
nne za polisi ziliendelea kupiga kambi kwenye Hoteli ya Land Mark kwa
zaidi ya saa moja kuhakikisha hatutoi tamko.
"Hata
hivyo, tutaendelea kuwasiliana na umma kupitia njia nyingine za
mawasiliano ili kupaza sauti zetu dhidi ya ukandamizwaji wa demokrasia
na haki za binadamu,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro alipotafutwa alisema uwapo wa polisi eneo la hoteli hiyo ni sehemu ya doria ya kawaida.
“Hivi polisi alipo watu wakimbie? Ebu wahoji hao kwa nini walikimbia. Sisi tutaendelea kuwapo na hata sasa ukienda mahotelini utaona polisi, je watu wanakimbia?” alihoji Muliro na kuongeza:
“Wewe si unaona polisi mitaani je watu wanakimbia? Waulizeni wao kwa nini walikimbia.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro alipotafutwa alisema uwapo wa polisi eneo la hoteli hiyo ni sehemu ya doria ya kawaida.
“Hivi polisi alipo watu wakimbie? Ebu wahoji hao kwa nini walikimbia. Sisi tutaendelea kuwapo na hata sasa ukienda mahotelini utaona polisi, je watu wanakimbia?” alihoji Muliro na kuongeza:
“Wewe si unaona polisi mitaani je watu wanakimbia? Waulizeni wao kwa nini walikimbia.”
Hata
hivyo, muda mfupi baadae, waandaaji hao walitoa taarifa yao ikiwa
imeorozesha waandaaji kuwa ni Taasisi za Umoja wa Kizazi cha Kuhoji
Tanzania (UTG), Kamati ya Mshikamano Kati ya Tanzania na Sahara
Magharibi (TASSC) na Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP).
Kwa
pamoja, mitandao hiyo kupitia kwa mratibu wao, Shao walieleza kuwa
wanaharakati wa haki za binadamu, asasi za kiraia na wananchi karibu
nchi zote za Afrika Mashariki wamekuwa wakishughulikiwa ili kuhakikisha
baadhi ya tawala zinatawala bila kikwazo.
Alisema
katika kufanikisha hilo, wapinzani wa serikali wanashambuliwa,
wanauawa, kubambikiwa kesi, kuozea jela bila hatia, kufilisiwa au
kuzuiwa nje ya nchi kwa fimbo ya uraia suala ambalo halipaswi kukaliwa
kimya.
Alisema
wamefadhaishwa na kushamiri kwa vitendo vya ukandamizwaji wa haki za
binadamu, kusiginwa kwa misingi ya kidemokrasia na utawala bora na
kuchipua kwa siasa za mkono wa chuma chini ya mtu mmoja badala ya
utawala wa taasisi za umma na vyombo vya uwakilishi wa watu.
Shao
alisema kwa Uganda, wameshtushwa na hatua ya hivi karibuni ya Serikali
ya Rais Museveni kumkamata, kumshikilia kwenye korokoroni ya kijeshi,
kumtesa na kumfungulia mashtaka bandia ya kukutwa na silaha Mwanamuziki
na Mbunge wa Jimbo la Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulani, maarufu kwa
jina la Bobi Wine.



No comments:
Post a Comment