Siku
moja baada ya makontena 20 yaliyo bandarini kwa jina la Paul Makonda,
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam kufanyiwa mnada na kukosa wateja,
amefanya ibada akiomba yakose wateja.
Juzi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilifanya mnada makontena hayo katika eneo la bandari kavu ya Malawi Cargo, lakini yalikosa wanunuzi baada ya waliojitokeza kushindwa kufika bei iliyotakiwa.
Jana Makonda alikwenda katika Kanisa la Anglikana wilayani Ngara, Mkoani Kagera ambako iliendeshwa ibada maalumu ya kuzuia mnada wa makotenda yenye samani za walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Makonda ambaye yupo kwenye msiba wa mama mkubwa wa mkewe, alishiriki ibada hiyo na aliwaambiwa waumini wa kanisa hilo kuwa amesali pamoja nao kwa sababu anaamini Mungu ndiye aliyempa makotenda hayo kwa ajili ya walimu wa Mkoa wake.
Alionya kuwa atakayenunua makontena hayo atalaaniwa yeye na uzao wake wote kwa sababu vya madhabahuni havichezewi.

“Nimekwenda
katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Anglikana mjini Ngara,
nimefanya ibada maalumu kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa
kuwa naamini Mungu alinipa kwa ajili ya walimu wa mkoa wangu,” anasema
Makonda.
RC
Makonda anadai kupatikana kwa samani hizo ni jitihada zake binafsi za
kuboresha mazingira ya kufanyia kazi walimu ikiwa ni kumuunga mkono Rais
John Magufuli aliyeamua kutoa elimu bure kwa Watanzania na hasa watoto
wa masikini.
“Rais
alitambua umuhimu wa elimu ndiyo maana kama msaidizi wake sikuona
sababu ya kukaa kimya wakati mazingira ya walimu si rafiki na kusubiri
kuwalaumu pale watoto wanapofeli bila kufanyia kazi changamoto zao.
“Baada
ya kuona jitihada za Rais katika sekta ya elimu, kwa kutoa elimu bure
nami nikawaza kama msaidizi wake, nafanya nini kuunga mkono kazi nzuri
anayoifanya Rais.”
“Ndipo
Mungu aliweka wazo lake ndani ya moyo wangu juu ya ujenzi wa ofisi za
walimu kama sehemu ya kuboresha mazingira yao. Kwa utukufu wake Mungu,
akaandaa watu wa kuchangia tena kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema
Makonda.
Akitumia
maneno ya vitabu vitakatifu, Makonda alisema utukufu wa Mungu
umejidhihirisha kwa Watanzania kuchangia, wakiwemo askari wa Jeshi la
Kujenga Taifa waliojitolea kujenga majengo; benki kwa kununua saruji;
baadhi ya viwanda kutoa mabati na nondo na wengine kujitolea masinki,
mabomba na taa.
Makonda
alisema nchi ya China imejenga ofisi, huku Watanzania wanaoishi
Marekani wakimpatia samani za walimu ambazo zipo kwenye makontena zaidi
ya 20 yaliyokwama bandarini yakidaiwa kodi.
“Wananchi na vyombo vya habari wamejitolea na kuendelea kuhamasisha, huku walimu wakichanga kama sehemu ya kujikomboa.
“Cha
kushangaza leo vinapigwa mnada ili kutoza kodi kwa kuwa tu makontena
yameandikwa Makonda basi kama jina langu hawalipendi watafakari mzigo
alionao mwalimu wa Dar es Salaam anayegombea kiti na mwanafunzi anayekaa
chini.
“Inasikitisha sana leo TRA inapiga simu kuomba shule binafsi zikanunue vifaa vilivyoletwa kwa msaada na Watanzania kwa ajili ya Watanzania wenzao.
“Ninachoweza kusema tu waliopewa madaraka wawe na hofu ya Mungu, mimi sikalii viti hivyo hata kama msingi wake ni chuki mchukieni Makonda lakini si walimu,” alisema Makonda.

alisema, “Nakuhakikishia atakayenunua hivi vifaa vya walimu amelaaniwa
yeye na uzao wake na kamwe hatafanikiwa katika maisha yake. Nayasema
haya nikiwa na uhakika kwa kuwa vya madhabahuni havichezewi.”

No comments:
Post a Comment