Katibu
Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi
katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani
Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
******
Na Stella Kalinga, Simiyu
******
Na Stella Kalinga, Simiyu
Katibu
Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema Mkoa wa Simiyu ni mkoa wa
kwanza katika utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mshikamano kati ya
Serikali na Chama Tawala.
Dkt.
Bashiru amesema hayo wakati akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi
katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani
Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
“
Simiyu ni Mkoa wa Kwanza kwa Tanzania Bara katika Utekelezaji wa Ilani
ya Chama Cha Mapinduzi, matokeo tunayoyaona, haya yanayotufurahisha
chanzo chake ni mshikamano baina ya Viongozi wa Chama na Serikali katika
Mkoa” alisema Dkt. Bashiru.
Wakati
huo Dkt. Bashiru ameitaja mikoa mitatu ikiongozwa na Simiyu ambayo
inafanya vizuri katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM kuwa ni pamoja na
Singida, Dodoma na Pwani, huku akieleza kuwa katika mikoa hiyo viongozi
na watendaji wa Chama wanafanya kazi kwa kushirikiana katika shida na
raha.
Aidha,
ameitaja mikoa minne ambayo haifanyi vizuri kuwa ni Mara, Arusha, Mbeya
na Dar es Salaam na akawataka viongozi wa Chama na Serikali katika
mikoa hiyo kujirekebisha ili waweze kufanya kazi kwa kushirikiana.
Amesema
Chama kimeumizwa sana na makundi na kinapata tabu pale ambapo viongozi
wa Chama na Serikali hawana mtazamo mmoja, hivyo amewataka viongozi wa
mikoa ya Mara, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam kushikamana na kuwa kitu
kimoja ili waweze kuwatumikia wananchi ipasavyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema uhusiano
kati ya Chama na Serikali kwa mkoa huo kuanzia ngazi ya Kijiji na Tawi
hadi mkoa uko vizuri na akimhakikishia Katibu Mkuu wa CCM kuwa
mshikamano baina yao utaendelea kuimarishwa.



No comments:
Post a Comment