Rais
Dkt. John Magufuli amempandisha cheo Kaimu meneja wa Kampuni ya huduma
za Meli (MSCL) Erick Hamis kuwa Meneja mkuu kwa kile alichodai kuwa
amependezwa na mikakati yake inayoonesha dhahiri nia yake ya kulifufua
shirika hilo na kumpa sharti la kutolewa sifa na kuliua tena shirika.
Rais
amefanya uamuzi huo wakati akihutubia wananchi na wafanyakazi wa
kampuni hiyo jijini Mwanza baada ya kushuhudia makubaliano rasmi ya
mkataba wa ujenzi wa Meli mpya Chelezo, na ukarabati wa Meli za MV
Victoria na MV Butiama katika ziwa Victoria na kampuni nne kutoka Korea
Kusini, mkataba ambao una thamani ya Shilingi bilioni 152.
Rais
Magufuli amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikielekea mwisho na alikuwa
mbioni kuifuta kama sio jitihada za kiongozi huyo kuonesha nia katika
kupambana na rushwa ambayo ndio kikwazo alichokitaja kuua vyanzo vya
mapato, hivyo kumuagiza meneja huyo kuhakikisha hakuna kitakachopotea
kuanzia leo anapokabidhiwa majukumu rasmi.
"Enzi
zile kulikuwa na wizi, wafanyakazi walikuwa wakiiba mafuta. Mapato
yalipokuwa yakipatikana yalikuwa yakipelekwa Dar es Salaam na
wafanyakazi wanafahamu". Rais Dkt. Magufuli.
Awali
akitoa taarifa ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa meli hiyo mpya na
ukarabati wa meli nyingine za MV Viktoria na Mv Butiama na ujenzi wa
Chelezo, Meneja huyo amesema ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba
abiria 1,200 yenye tani 400 utatoa ajira 250.
No comments:
Post a Comment