Barua ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), kuomba kujiuzulu imezua mjadala mzito ndani ya chama hicho.
Kubenea
anadaiwa kuandika barua kuomba kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa
Chadema Kanda ya Pwani, jambo ambalo linaonekana kuleta mgongano na
kurushiana mpira.
Wakati
mjadala huo ukishika kasi hadi sasa mbunge huyo hajakubali wala kukataa
kuhusu barua hiyo aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicent
Mashinji ambaye anasema pindi itakapomfikia ataifanyia kazi haraka.
Barua
hiyo ya Agosti 28 mwaka huu ilianza kusambaa mitandaoni juzi, ambapo
Kubenea alikuwa akitoa utetezi wake kutokana na kuandikiwa barua na na
Katibu Mkuu wa chama hicho akitakiwa kujieleza kwanini asichukuliwe
hatua za kinidhamu kwa kusababisha migogoro kupitia mitandao ya kijamii.
Katika
barua hiyo yenye kumbukumbu MB/U/CDM/018/1 kwenda Ofisi ya Katibu Mkuu
wa chama hicho, Kubenea alitakiwa kujibu tuhuma tano dhidi yake.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk. Mashinji alikiri kuona
barua ya mbunge huyo kupitia mitandao ya kijamii, huku akiweka wazi
kwamba pindi itakapomfikia ataifanyia kazi kwa haraka.
“Barua
hiyo kama ambavyo umesema mwandishi ipo mitandaoni mimi bado sijaiona
na kama nikiiona nitaifanyia kazi,’’alisema Dk. Mashinji.
Katika
kile kinachooneka kuwa ni kukosekana kwa ufafanuzi wa kina Kubenea
alikiri kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho ikimtaka
kujieleza kutokana na kikao cha Kamati Kuu (CC) iliyokutana Julai 7 na 8
mwaka huu.
Katika
sehemu ya majibu ya Kubenea kwa Katibu Mkuu alieleza kukiri kupokea
barua iliyoelekezwa kwake Julai 19 mwaka huu 2018 yenye Kumb. Na.
C/HQ/K/PWN/MG/30/8, kuhusu “KUJIELEZA KWA KATIBU MKUU”
No comments:
Post a Comment