Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelaani tukio lililofanywa na
Mgambo wa Jiji la Dar es salaam akisema ni la kihuni, kishenzi na
kinyama na halipaswi kufumbiwa macho na wapenda amani, watetezi wa haki
za binadamu na wananchi wote kwa ujumla.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Kamanda wa polisi
Mkoa wa Mwanza, Lugola alisema Serikali inalaani vikali tukio hilo
ambalo lililotokea wiki iliyopita jijini humo, na kutokana na unyama huo
tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa.
“Jeshi
la Polisi tayari limewakamata wahusika kama Taarifa ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni tarehe 31 Agosti, 2018 ilivyoeleza. Natumia
fursa hii kuwakumbusha tena Mgambo wote kuwa makini katika utekelezaji
wa maagizo wanayopewa na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu,” alisema
Lugola.
Pia
kutokana na tukio hilo, Lugola alisema anazitaka Mamlaka za Majiji,
Manispaa na Halmashauri kufikiria kuanzisha Huduma ya Polisi Wasaidizi
(Auxiliary Police) katika maeneo yao kwa mujibu wa Sheria ya Polisi na
Polisi Wasaidizi Sura ya 322 ili kuepuka matukio ya uvunjifu wa haki za
Binadamu kama tukio la Mgambo watatu jinsi lilivyo tokea.
Aidha,
Lugola pia alizungumzia kuhusu baadhi ya matukio mengine ambayo watu
wanajichukulia Sheria mkononi na kuwaadhibu kwa kuwapiga watu wengine
kwa sababu mbalimbali.
Aliyataja
matukio hayo ni pamoja na ugomvi wa kifamilia ndani ya ndoa ambao
huhusisha Wanaume kuwapiga wake zao au wake kuwapiga waume zao, pia
wananchi kuwapiga watu wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali, pamoja na
walimu kuwapiga wanafunzi kinyume cha sheria.
Pia
Lugola aliwaonya baadhi ya Askari Polisi ambao wanatumia nguvu isiyo ya
kadiri kulingana na mazingira halisi wanapowadhibiti watuhumiwa.
“Serikali
kupitia Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalaani vikali
matukio ya kujichukulia Sheria mkononi na kupitia kwenu Wanahabari
nawataka Watanzania kufuata sheria za nchi kwa kuacha vitendo vya
kujichukulia Sheria mkononi. Vitendo hivi pamoja na kusababisha uvunjifu
wa amani vinaweza kuleta madhara kwa watu ambao hawana makosa na
kuichonganisha Serikali na wananchi wake,” alisema Lugola.
Kutokana
na matukio hayo, Lugola aliwataka wanandoa wanakumbushwa kutumia Dawati
la Jinsia katika Vituo vya Polisi kote nchini ili kuwasilisha
malalamiko yao ya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya ndoa ili hatua
stahiki zichukuliwe.
Pia
aliwataka wananchi waendelee kuheshimu sheria za nchi na kuepuka
kujichukulia unakuta mtu anapigwa hata haulizi anayepigwa amekosa nini
nae anajiunga nao na kumpiga hali ambayo imesababisha majeraha, vilema
vya kudumu na vifo kwa watu wasio na hatia.
Hata
hivyo, Lugola aliwaonya walimu kwa kufanya matukio kujirudia kwa
kuwaadhibu wanafunzi kwa kuwachapa na kuwapiga hovyo kiasi cha
kusababisha maumivu makali, ulemavu na vifo.
“Natumia
fursa hii kuwakumbusha Walimu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na
Miongozo ya Adhabu kwa wanafunzi ambayo imetolewa na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia ili kuepuka madhara yake, kuondoa hofu kwa wazazi
na kufanya shule zetu kuwa mahali salama kwa watoto wetu,” alisema
Lugola.
No comments:
Post a Comment