Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kitendo cha Asia Msangi kujitokeza kugombea ubunge Ukonga ni ujasiri ambao unatakiwa kuungwa mkono kabla hata hajasema atafanya.
Lema
ameyasema hayo jana Septemba 2, 2018 kwenye kampeni za Chadema
zilizofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chanika, jijini Dar es
Salaam.
Alisema wanaume wa Dar es Salaam wamekuwa ni waoga na wanarubuniwa na fedha au kuahidiwa vyeo.
Alisema yeye ataendelea kupigania haki za wanyonge licha ya vitisho vingi dhidi ya wapinzani.
Lema
ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amewataka wakazi wa Chanika
kumchagua mgombea huyo ili akaungane naye kwenye harakati za kujenga
demokrasia.
Alisema
Chadema imeibiwa kura kwenye chaguzi za Kinondoni na Siha, hivyo
amewataka siku ya uchaguzi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kulinda
kura zao.
"Hamna
dhambi kubwa kama uoga, msitishwe na hawa polisi, ninyi mna nguvu kubwa
kuliko wao. Uchaguzi huu si kati ya Asia na Mwita bali ni kati ya nuru
na giza," alisema Lema.
Mbunge huyo amesema vita inayoendelea ni ya demokrasia dhidi ya watu wanaotumia nguvu kubwa kuua demokrasia ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment