Mgombea
ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Ukonga
jijini Dar es salaam Asia Msangi amesema miongoni mwa changamoto
anazokutana nazo kuelekea uchaguzi wa marudio jimbo hilo utakaofanyika
siku ya jumapili ya septemba 16, ni hofu ya kutekwa na watu
wasiojulikana.
Akizungumza
katika kituo cha EATV leo, mgombea huyo wa CHADEMA amesema kupitia
viongozi wa juu wa chama chake wamepokea taarifa juu ya uvumi wa kutaka
kutekwa siku moja kabla ya zoezi la kupiga kura.
“…Baadhi
ya changamoto kwenye uchaguzi huu wa marudio ninazokutana nazo .., kuna
baadhi ya watu wetu wanatishiwa kutekwa na kuna mwingine alitekwa ila
kwa ushirikiano na mwenyekiti jana amepatikana.., lakini pia kupitia
viongozi wa juu wa chama tumepokea taarifa ya mimi kutaka kutekwa kabla
ya jumamosi na hili jambo tutalifikisha polisi. ” Amesema Asia Msangi
Aidha
Asia Msangi amesema licha ya miradi mbalimbali ya maendeleo
inayotekelezwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia seikali ya awamu ya
tano ikiwemo reli ya kisasa (SGR), ununuaji wa ndege pamoja na Shirika
la ndege la Tanzania ATCL anaamini miradi hiyo haiwezi kuwa kikwazo cha
kutoshinda uchaguzi wa jimbo hilo.
“
Licha ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Rais Magufuli bado
maisha ya mwananchi mmoja mmoja wa jimbo la ukonga ni magumu.., hiyo
miradi haiakisi chochote.., wananchi wa ukonga hawawezi
kunufaika..”Ameongeza Asia Msangi
Uchaguzi
wa jimbo la Ukonga unarudiwa kufuatia aliyekua Mbunge wa jimbo hilo
kupitia CHADEMA Mwita Waitara kutangaza kujivua nafasi hiyo Julai 28
mwaka huu kwa madai ya kuwa na mgogoro na Mwenyekiti wa chama hicho
Freeman Mbowe.
No comments:
Post a Comment