Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), inatumia kati ya Sh. milioni 450 hadi Sh.
milioni 600 kila mwezi kugharamia wagonjwa wanaoshindwa kulipia matibabu
yao.
Hayo
yalielezwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili,
Profesa Lawrence Museru alipokuwa akimkabidhi msaada wa baiskeli ya
matairi matatu, Said Mtonga ambaye amekatwa miguu yote miwili kutokana
na maradhi yanayomsumbua.
“Jukumu
letu ni kutibu lakini inapobidi huwa tunaenda zaidi ya hapo na kutoa
msaada ‘rehabilitation’, kwa mgonjwa kama huyu, ili anapotoka hapa aweze
kwenda kuendelea na majukumu yake, ajenge uchumi wa nchi na wake pia.
“Hivyo,
hospitali imegharamia matibabu yake yote kwa kuwa hakuwa na uwezo wa
kulipia na kwa mwezi huwa tunatumia kiasi cha kati ya Sh. milioni 450
hadi Sh. milioni 600,” alisema.
Ofisa
Ustawi wa Jamii Muhimbili, Wodi ya Kibasila, John Mwakyusa alisema
matibabu ya Said yamegharimu Sh. 935,000 tangu alipofika hospitalini
hapo Mei, mwaka huu. .
“Alikukuja
miguu yake ikiwa imevimba na ina vidonda, alichunguzwa na kuonekana
haikuwa saratani, madaktari wakamfanyia upasuaji kukata mguu wake mmoja
lakini baadae mguu uliobaki nao ulionyesha tatizo, nao ukakatwa.
“Ndugu
zake hawakuwahi kujitokeza, tukawatafuta lakini tulipowapata
walitueleza hawakuwa na uwezo wa kumsaidia, hata marafiki zake pia
hawakuja,” alisema.
Alisema waliendelea kumtibia hadi alipopona kabisa wakaona ni vema kumtafutia baiskeli ili aweze kutembelea.
“Tunamshuruku mkurugenzi alitupatia Sh. 500,000 tukaenda SIDO kutafuta Sh. 80,000 tukampa mtaji,” alisema.
Mkuu
wa Idara ya Ustawi wa Jamii Muhimbili, Emmanuel Mwasota alisema ugonjwa
uliokuwa ukimsumbua Said kitaalam unaitwa Septic Wound with Gangrene.
No comments:
Post a Comment