Rais
Magufuli ameyasema hayo jana, kwenye mkutano wa hadhara aliofanya
wilayani Meatu mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa
ya kanda ya ziwa ambapo amesisitiza watanzania waendelee kuzaa lakini
wachape kazi ili kuwatimizia mahitaji muhimu watoto wao.
''Najua
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu hapa angependa kuongelea mambo ya uzazi wa
mpango lakini mimi mengine huwa sikubaliani nayo sana, utapangiwaje
kuzaa'' ? alihoji Rais katika mkutano huo.
Rais
Magufuli alisema amezunguka mataifa mengi duniani na amejionea jinsi
yanavyotafuta nguvu kazi kutokana na mambo ya uzazi wa mpango hivyo
kuwashauri wananchi kusikiliza na kuchuja baadhi ya mambo.
''Kwahiyo
katika kushauriwa mengine tukubali na mengine tukatae tutumie msemo wa
mzee Jakaya Kikwete (Ukiwambiwa changanya na za kwako) kuzaa ni
muhimu'', amesema.
Aidha
alisisitiza kuwa anajua watapinga sana lakini ukweli ndio huo watu
wamejazwa mawazo ya ajabu na kwamba huwezi kuwa mwanaume kisha ukubali
kufungiwa kizazi.
No comments:
Post a Comment