Rais
John Magufulia amewaambia wakazi wa Itilima mkoani Simiyu wachape kazi,
huku akisisitiza kuwa Serikali haitatoa chakula cha bure.
Rais
Magufuli ameyasema hayo jana Septemba 9, ikiwa ni siku ya pili ya ziara
yake mkoani Simiyu akitokea Mara. Amewataka wananchi hao kutafuta
maendeleo ya kweli hasa kwenye kilimo ambacho ndiyo shughuli kuu ya
uchumi wao.
“Endeleeni
kuchapa kazi, chakula cha bure hakitakuja. Hili lazima niwaambie
ukweli, Serikali haina shamba,” alisema Rais Magufuli aliposimama na
kuzungumza na wakazi hao.
Rais
Magufuli amewataka pia kuachana na imani za kishirikina badala yake
wapeleke watoto wao shule kwa sababu Serikali inatoa elimu bure.
“Kila
mwezi tunatoa Sh23.85 bilioni kwa ajili ya elimu bure. Pelekeni watoto
shule,” alisema Magufuli huku akishangiliwa na wananchi hao.
No comments:
Post a Comment