Na Mathias Canal (WK), Dodoma
Kumalizika
kwa Mkutano wa Mapinduzi ya kijani Barani Afrika (AGRF 2018) mjini
Kigali nchini Rwanda kumeongeza tija na ufanisi kifikra kwa washiriki
ikiwemo Tanzania kwa kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa na mafanikio
chanya kiuchumi kulingana na rasilimali zake nyingi za asili ikiwemo
ardhi yenye rutuba katika kilimo.
Afrika
ina hekta milioni 600 za ardhi isiyozalishwa ambayo ni sawa na asilimia
60 ya jumla ya kimataifa. Waziri wa kilimo Tanzania-Mhe Dkt Charles
Tizeba anaamini kwamba mafanikio katika kukuza na kuimarisha uchumi
Barani Afrika ni kupitia kilimo hivyo msisitizo mkubwa ni kusimamia
kiufasaha mikakati inayowekwa kwenye sekta hiyo kuliko mijadala pekee.
Anasema
Afrika inakadiriwa kuwa na idadi kubwa kufikia bilioni mbili mwaka wa
2030 hivyo mapinduzi ya kilimo yanapaswa kuimarisha mahusiano ya
serikali na wananchi kwa kuwatunza wakulima kama wateja na kuwapatia
ujuzi na huduma bora ili kuongeza uzalishaji wa Mazao yao.
Kurejea
kwa waziri wa kilimo Mhe Tizeba jana tarehe 9 Septemba 2018 kunamfanya
kuendelea na majukumu nchini mwake akiwa na fikra chanya kupitia tukio
la kila mwaka la kongamano la Mapinduzi ya kijani (AGRF) linalowaweka
pamoja wakuu wa nchi, wajasiriamali, wataalamu wa sekta na wakulima kwa
mazungumzo muhimu juu ya hali ya kilimo barani Afrika.
Waziri
huyo wa kilimo nchini Tanzania alipochangia mjadala kuhusu upotevu wa
chakula baada ya uvunaji alisema jambo hilo limeendelea kuwa tatizo
kubwa siyo tu katika chakula lakini pia katika malighafi kwa maendeleo
ya viwanda huku akizitaja juhudi zilizofanywa na serikali ya Tanzania
kupunguza upotevu wa chakula.
Dkt
Tizeba, alielezea juhudi hizo kuwa ni pamoja na kushirikiana na wadau
mbalimbali wa maendeleo, taasisi za kimataifa kama vile Bill and Melinda
Gates foundation, HELVETAS Swiss Inter Cooperation Agency, Rockefeller
foundation, AGRA, shirika la chakula Duniani, mashirika yasiyo ya
kiserikali ambayo yameboresha kwa kiasi kikubwa teknolojia ya uhifadhi
kama vile mifuko ya plastiki ya kuhifadhia nafaka ambayo imeonesha kuwa
na mafanikio makubwa sana kwa kuzuia wadudu waharibifu kupenya na
kushambulia nafaka.
Sambamba
na hilo alisema juhudi za kupambana na upotevu wa chakula kumeifanya
Tanzania kuanzisha mfumo wa kubadilishana bdhaa. Kuweka mazao katika
masoko yaonekanayo ili kurahisisha uuzaji na kupunguza upoteaji wa
bidhaa za kilimo. Chini ya mradi huu mazao yatatunzwa chini ya mfumo wa
vikundi vya wakulima na kuuzwa moja kwa moja katika mfumo wa kupitia
soko la bidhaa.
Kongamano
hilo limefika ukomo hapo jana tarehe 8 Septemba 2018 baada ya kujadili
maswala ya kilimo kwa siku nne mfululizo, lilihudhuriwa pia na viongozi
wengine wa Afrika akiwemo Rais wa Ghana Mhe Nana Addo Dankwa Akufo Addo,
Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto, Waziri Mkuu wa Gabon Mhe
Emmanuel Issoze-Ngondet sambamba na Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza Mhe
Tony Blair.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment