Serikali imesema haitawalipa watumishi waliofukuzwa kazi kwa kuwa na vyeti feki kutokana na udanganyifu huo.
Akijibu
swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Aida Khenani bungeni
jijini Dodoma leo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala
Bora, George Mkuchika amesema serikali haijapanga kumlipa mtumishi
yeyote ambaye mkataba wake ni feki.
Akiuliza
swali hilo, Aida amesema kabla ya kupunguzwa kwa watumishi hao
waliodaiwa kuwa na vyeti feki, serikali ilikuwa na vyeti feki na hadi
sasa kuna upungufu wa watumishi wa kiasi gani.
“Serikali
ya Tanzania inathamini zaid vyeti kuliko taaluma, kuna wengine walikuwa
wamebakisha mwaka mmoja tu ili wastaafu, je, serikali ina mpango gani
wa kuwalipa watumishi hao,” amesema.
Mkuchika
akijibu hilo amesema; “Mwajiri alikuajiri akijua vyeti ulivyompelekea
ni sahihi, kitendo cha kumdanganya kinafuta mkataba wenu na serikali
haijapanga kuwalipa watumishi wa aina hiyo,”
Katika
swali lake la msingi, Aida alitaka kujua mkakati wa serikali kuziba
nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliokumbwa na sakata la vyeti feki
ambapo Waziri Mkuchika alijibu serikali imeshatoa kibali cha kuajiri
watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo la lililosababishwa na
kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi wa umma
waliobainika kughushi vyeti.
==>>Tazama video hapo chini
==>>Tazama video hapo chini
No comments:
Post a Comment