Serikali imesema imesitisha uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala hadi yaliyopo yaimarishwe kikamilifu.
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Josephat Kakunda, amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo
Jumatatu Septemba 10, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini,
Daimu Mpakate ambaye alihoji mpango wa serikali kuigawa Halmashauri ya
Wilaya ya Tunduru, mkoani Mtwara ambayo ina wilaya sita.
Akiuliza
swali hilo bungeni jijini Dodoma jana, mbunge huyo amesema;
“Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru iliomba kuigawa wilaya hiyo ambayo ni
kubwa zaidi mkoani humo ikiwa na wilaya sita, kata 39 na vijiji 167, je
serikali ina mpango gani wa kuigawa ili iwe rahisi katika kutoa huduma
karibu zaidi na wananchi.”
Kajibu
swali hilo, Kakunda amesema suala hilo lina changamoto ya kuimarisha
kwanza miundombinu kama majengo ya ofisi, nyumba za watumishi na
mahitaji mengine kama vifaa, watumishi wa kutosha na vyombo vya usafiri
kwenye maeneo mapya ya utawala tangu mwaka 2010 na 2012.
“Maombi
ya kugawa Wilaya ya Tunduru na kuanzisha Halmashauri ya Wilaya ya
Busanda, yaliwasilishwa Tamisemi yakiwa na ombi la kuanzisha Mkoa mpya
wa Selous. Serikali imetafakari maombi hayo na kuyaona ni ya msingi
lakini yana changamoto nilizoainisha awali,” amesema Kakunda.
No comments:
Post a Comment