Spika
wa Bunge, Job Ndugai amekerwa na wabunge wa CCM na Mawaziri kutotumia
mitandao ya kijamii kupeleka majibu na ufafanuzi wa Serikali kwa
wananchi kama wafanyavyo wapinzani.
Ndugai
alieleza hisia zake jana Septemba 10, 2018 akisema wabunge wa upinzani
wamekuwa wajanja katika kutumia mitandao ya kijamii ambayo inasomwa
dunia nzima na hivyo kuwaaminisha watu.
Alitoa kauli hiyo wakati Bunge likipitisha muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 wa 2018.
"Kuna
katabia kamezuka humu, wabunge wanaishambulia Serikali lakini inapokuja
muda wa kujibu wanakuwa hawapo, lakini wanakuwa wameshashinda maana
wanakuwa wametuma kwenye YouTube na watu dunia nzima wanasoma lakini
ninyi (wabunge wa CCM) hakuna, utakuta hata ufafanuzi wa mawaziri
hakuna," alisema Ndugai.
Alisema
ni wakati sasa wabunge wa CCM na mawaziri kujipanga na kutumia mitandao
ipasavyo ili dunia ijue mambo mazuri ya Bunge la Tanzania na hapo ndipo
watu watapata ufafanuzi kwa maswali ya upande wa pili.
No comments:
Post a Comment