Makamu
wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema wananchi wasitegemee kupelekewa
fedha Sh. milioni 50 walizoahidi mwaka 2015 katika kipindi cha uchaguzi
kwa kila kijiji.
Ameyasema
hayo jana Septemba 10, 2018, katika mkutano wa hadhara katika Kijiji
cha Kazuramimba wilayani hapa mkoani Kigoma, kwamba hawatapelekewa fedha
hizo na badala yake zitapelekwa kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema
kuliko kuwapa fedha hizo kwa kila kijiji Serikali imeamua kuwekeza
katika elimu, afya, barabara pamoja na maji lengo ni kupeleka maendeleo
katika nchi.
"Serikali ya awamu ya tano imeamua kujitegemea katika kujitegemea lazima tujiwekee mikakati kuleta maendeleo katika nchi yetu.”
“Tumeanza
kuwekeza katika maswala ya usafiri wa anga na nyie ni mashahidi
mmeshuhudia tukinunua ndege zetu," alisema Samia Suluhu
Alisema
Serikali imeamua kujitegemea lakini sio kujitegemea asilimia miamoja,
kwani wataendelea kuhitaji misaada lakini kuna changamoto au vipaumbele
vya kitaifa katika vipaumbele hivyo pesa itakayo patikana itashuka hadi
kwa mwananchi wa chini.
"Tumeamua
kujenga reli itakavyokuwa inaenda haraka na kubeba mizigo mingi zaidi
na ikifanya kazi faida yake itafika mpaka kwa wananchi wa chini,”
alisema
Alisema
Serikali imeamua kuweka umeme mkubwa utakaowaka nchini nzima bila
kuzimika ambao utatumika kwenye viwanda vitakavyojengwa Tanzania na
faida yake itawafikia wananchi wote.
"Fedha hizo ambazo tumesema tutawapa katika kila kijiji tungeweza (kugawa) kwa kila mtu tusingeweza kuona faida yake.”
“Kwa
hiyo sisemi tunaifuta ahadi yetu ipo kwenye ilani ya uchaguzi chama
kimetuagiza ni wajibu wetu Serikali kutekeleza, lakini maendeleo kuna
kupanga na kuchagua katika mipango yetu ya sasa hivi, hilo tumeliweka
pembeni kwanza," alisema makamu huyo.
Alisema
wasikae na kudanganya watu kwamba kuna fedha hizo zinatoka serikalini
zinakuja zitaingizwa katika miradi muhimu kuliko kuwapa fedha mkononi na
ukizingatia serikali inatoa fedha nyingi katika kuhudumia sekta ya
elimu.
No comments:
Post a Comment