Serikali
imesema sekta binafsi wanaruhusiwa kuwalipa watumishi wake zaidi ya
kiwango cha kima cha chini cha mshahara pale ambapo wanaona kufanya
hivyo itaongeza motisha kwa wafanyakazi wao.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu
Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, amesema bungeni jijini Dodoma leo
Jumanne Septemba 11, akijibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema (Chadema), aliyeuliza katika kipindi cha na maswali na majibu
bungeni endapo serikali haioni haja ya kuboresha mishahara yake na
kuzielekeza sekta binafsi kulipa mishahara inayoendana na hali ya
maisha.
Akijibu
hilo Mavunde amesema, serikali imeweka utaratibu kwa waajiri na
wafanyakazi katika sekta binafsi, kujadiliana na kufunga mikataba ya
hali bora mahali pa kazi kwa lengo la kuboresha maslahi yao ikiwamo
mshahara na stahiki nyingine.
“Kupitia
utaratibu huu, sekta binafsi wanaruhusiwa kulipa zaidi ya kima cha
chini ili kuwafanya wafanye kazi kwa bidii na kujituma kwa lengo la
kuzalisha mali au katika ktoa huduma.
“Hata
hivyo, pia Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7, ya mwaka 2004 kama
ilivyorekebishwa mwaka 2015, imeanzisha Bodi ya Mishahara ya sekta
binafsi ambayo ina jukumu la kufanya utafiti kwa kuzingatia hali halisi
ya gharama za maisha na masuala mengine ya kiuchumi na kupendekeza
kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi,” amesema.
Pamoja
na mambo mengine, Mavunde amesema serikali iko katika hatua za mwisho
za kuiwezesha bodi hiyo kufanya utafiti kuhakikisha utafiti huo unakidhi
matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu zinazokubalika nchini na viwango
vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment