Ushahidi
wa kesi inayomkabili mbunge wa Kawe, Halima Mdee haukusikilizwa leo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mshtakiwa (Mdee) katika kesi
hiyo kudaiwa anaumwa.
Hayo yameelezwa leo Septemba 11 na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Akizungumza
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Mutalemwa amesema kesi hiyo
ilipangwa kusikilizwa leo Septemba 11 kwa mashahidi wa upande wa
mashtaka kutoa ushahidi lakini mshtakiwa hayupo akidaiwa kuumwa
Baada ya Kishenyi kueleza hayo, mdhamini wa Halima Mdee, Fares Robinson aliieleza mahakama kuwa anaumwa.
Hakimu
Simba baada ya kusikiliza Maelezo ya upande hizo zote aliipanga kesi
hiyo kusikilizwa tena Oktoba 8, mwaka huu ambapo mashahidi wa upande wa
mashtaka wataendelea kutoa ushahidi wao.
Katika
kesi hiyo mashahidi wawili wa upande wa mashtaka tayari wamekwishatoa
ushahidi wao ambao ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ilala(RCO), Davis
Msangi na Mkuu wa Kituo cha polisi cha Urafiki,Mrakibu wa Polisi
Batseba Kasanga.
Mdee alifikishwa mahakamani hapo kwa Mara ya kwanza Julai 10, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment