KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 5, 2018

TANZIA: MTAFITI BINGWA WA AFYA YA MAMA NA MTOTO DR. MBARUKU AAGA DUNIA



Mkurugenzi na wafanyakazi wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) wanasikitika kutangaza kifo cha
mfanyakazi mwenzao DK. Godfrey Mbaruku kilichotokea ghafla siku ya tarehe 2 Septemba 2018
nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Mpaka mauti yanamfika Dr. Mbaruku alikuwa
Mtafiti Mkuu kwenye miradi. Dr. Mbaruku aliwahi kuwa Naibu Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya
Afya Ifakara kati ya 2009 na 2015.


Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani na mazishi yanatarajia kufanyika Dares Salaam siku ya
Jumatano tarehe 5/09/2018 katika Makaburi ya Kinondoni.


Uongozi wa Taasisi ya Afya Ifakara unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, wafanyakazi na
wadau mbali mbali wa afya kwa msiba huu mkubwa.

                         IMETOLEWA NA IDARA YA RASILIMALI WATU

                                     TAASISI YA AFYA IFAKARA

                                         MIKOCHENI, DAR ES SALAAM

                                                 Septemba 4, 2018

No comments:

Post a Comment