Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhadisi Mshamu Munde akizungumza na Ripota maalum wa Globu ya Jamii leo kuhusu wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba unaoanza kesho Jumatano 5-6 Septemba wasimamiee kwa weledi na wanafuzi wafanye kwa waminifu.
Mitihani ya taifa ya darasa la saba inatarajiwa kuanza kesho nchini kote hivyo walimu wameombwa kusimamia mitihani hiyo vizuri na wale watakaokiuka sheria za usimamizi wa mitihani hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao huku zaidi wanafunzi 6000 watafanya mtihani huo.
Akizungumza Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid amesema kesho wanafunzi wa darasa la saba nchi nzima wanafanya mtihani wao wa mwisho kwahiyo amewaomba walimu wanaosimamia mitihani hii wafanye kazi yao kwa uadilifu na kufuata sheria muache udanganyifu.
Aidha amewataka wanafunzi kuwa watulivu katika pindi chote cha mitihani ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao hiyo nakuiletea sifa wilaya ya Mkuranga."Mwaka Jana Mkuranga tulishika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Pwani naamini tunaweza pia kuwa wa kwanza kitaifa kama wanafunza watatumia nafasi ya kesho kufanya mitihani vizuri"alisema Abeid
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa halmashauri hiyo imejiandaa vizuri kwani mpaka sasa vifaa vyote vinavyohusiana na mitihani vimeshakamilika."mandalizi ya mitihani yanahusisha vifaa vya mitihani,na mafunzo kwa wasimamizi wote wa mitihani vyote vimakailika ikiwemo masurufu,usambazaji wa mitihani na magari"alisema
Alisema kuwa zoezi hilo ni la kitaifa na serikali imewekeza fedha nyigi kwahiyo anawasihi wasimamizi wawe waadilifu wasijihusishe na vitendo vya udanganyifu wataitia serikali hasara kwa sababu imetumia pesa nyingi na kutoa rai kwao wafanye kazi kwa weledi.
Aidha alitoa wito kwa wanafunzi kufanya mitihani yao kwa uaminifu mkubwa wadifanye udanganyifu wa aina yeyote ile kwani utawaletea hasara kubwa
Hata hivyo zaidi ya wanafunzi 6000 wilayani mkuranga wanatarajiwa kuanzĂ mitihani wao wa mwisho wa kumaliza Elimu ya msingi hapo kesho
No comments:
Post a Comment