Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka mitatu jela ama kulipa faini
ya Sh. 24 milioni wafanyabiashara wawili wa madini baada ya kukiri kosa
la kukutwa na madini ya Coloured Gemstones yenye thamani ya Dola za
Kimarekani 1.8 milioni.
Pia
mahakama hiyo imeamuru madini hayo yataifishwe. Hata hivyo, washtakiwa
hao wameweza kuepuka kutumikia kifungo hicho baada ya kulipa faini hiyo.
Hukumu
hiyo, imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire baada ya
Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande kuwasomea mashtaka mawili
washtakiwa hao ambapo walikiri makosa yao.
Baada
ya kukiri makosa yao, Mahakama iliradhimika kuhamia maeneo ya Msasani
Kinondoni Dar es Salaam ambapo vielelezo vya kesi hiyo vilikuwepo,
ambapo kesi iliendeshwa na washtakiwa kutiwa hatiani. Washitakiwa hao ni
Aazam Nazim (Raia wa India) na Ango Mbossa raia wa Tanzania.
Hakimu
Rwizire hivyo alimtaka kila mshtakiwa kulipa faini ya Sh. 6 milioni kwa
kila kosa ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela katika kila kosa.
Kwa
kuwa kila mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili hivyo kila mshtakiwa
atapaswa kutoa faini ya Sh. 12 milioni iwapo atashindwa atatumikia
kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuwa vifungo hivyo vinaenda sambamba.
Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa yao kati ya January 2017 na June 2018 katika maeneo ya Misisiri A eneo la Mwananyamala.
Wanadaiwa kukutwa na madini aina ya Coloured Gemstones kilogramu 75,920.04 yenye thamani ya Dola za Kimarekani 1,795,687.87.
No comments:
Post a Comment