WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewatakaWatanzania waishio nje ya nchi
wahakikishe wanashiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao kwa
kushawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa waje kuwekeza nchini na
kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.
Amesema
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli
inaamini kuwa Tanzania itapata maendeleo makubwa ya kiuchumi endapo
wananchi wake watatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Hapa Kazi tu”.
Aliyasema
hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakatiakizungumza na
Watanzania waishio nchini China kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzani
uliopo jijini Beijing.
Alisema
nchi zote zilizoendelea zilihakikisha kuwa wananchi wake wanaelewa na
kutekeleza matamko yanayowahamasisha kufanya kazi, hivyo alitumia fursa
hiyo kuwahamasisha Watanzania popote walipo kutekeleza kwa vitendo
kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu.’
Waziri
Mkuu alisema China ambayo imefanikiwa kuwa moja kati ya nchi zenye
nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, imefika hapo kutokana na mchango
mkubwa uliotolewa na wananchi wake, ambao waliamua kuunga mkono juhudi
za Serikali yao kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi wakiwa ndani au nje
ya nchi.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nje ya nchi
wajiepushe na vitendo vya uhalifu hasa biashara ya dawa za kulevya
ambayo inachafua jina na heshima ya nchi yao kimataifa.
“Tanzania
ni nchi nzuri na inaheshimika duniani, nawasihi wote mnaoishi nje
muachane kabisa na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa sababu
inalitia doa Taifa na adhabu yake katika baadhi ya nchi ni kifo,”
alisisitiza Waziri Mkuu.
Awali,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt.
Augustine Mahiga alisema mwelekeo wa Diplomasia ya Tanzania Kimataifa
hivi sasa ni kiuchumi (economic diplomacy), hivyo Watanzania waishio nje
wanapaswa kuwa wabunifu, makini katika kutafuta fursa zenye manufaa kwa
nchi yao.
Alisema
Diplomasia ya Uchimi si kupeleka Tanzania wawekezaji tu bali wawekezaji
katika viwanda ambavyo kila vinapojengwa vinachangia kuinua uchumi wa
Taifa.
Kwa
upande wake,Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwaasa
vijana kuitumia teknolojia ya mawasiliano na mitando ya jamii kutafuta
habari na taarifa muhimu hasa nafasi za masomo ili kujiendeleza kielimu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 03, 2018.
No comments:
Post a Comment