WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesemalishe duni pamoja na ulaji usiofaa na
mitindo ya maisha vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la
magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususan kwa vijana na watu wazima, ambao
ndiyo nguvu kazi kwa Taifa.
“Ni
jambo lisilopingika kuwa hatua za kukabiliana na magonjwa ya kusendeka
(mfano matatizo ya moyo, saratani, kisukari na shinikizo kubwa la damu)
zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kasi ya maendeleo yetu
kwani gharama za matibabu yake ni kubwa mno; si kwa kaya zinazoathirika
tu bali kwa Taifa zima.”
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 11, 2018), wakati
akifungua mkutano wa tano wa wadau wa masuala ya lishe, uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu amesema lishe iliyozidi inadhihirishwa na ongezeko kubwa la
magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha
na ulaji usiofaa kama vile uzito uliozidi, viriba tumbo, shinikizo la
damu pamoja na kisukari.
Amesema
kasi ya ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza inapaswa
kudhibitiwa kwa kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha. “Huu
ni wakati wa kuangalia kwa pamoja kama jitihada zetu zinaleta matunda
tunayotarajia.”
Waziri
Mkuu amesema Serikali inatambua kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo
ya Taifa letu hivyo, uwepo wao katika mkutano huo unaonesha umuhimu wa
kuimarisha ushiriki wa kila sekta, kila mdau ikiwemo sekta binafsi kwa
nafasi yake katika kupambana na aina zote za utapiamlo.
Amesema
ushiriki wa kila sekta ni wa muhimu kwa sababu hakuna sekta moja pekee
inayoweza kuondoa tatizo la utapiamlo, pia ni vema kwa wadau hao
wakajitathmini mmoja mmoja katika sekta zao kuona kama wanaelekea katika
muelekeo sawa na mipango ya Serikali.
“Kwa
kuzingatia hilo, ofisi yangu imeweka utaratibu maalum wa kuratibu
utekelezaji wa kazi za lishe nchini, ambapo kamati ya Kitaifa ya
Usimamizi na Ushauri kuhusu masula ya lishe nchini yaani High Level
Steering Committee on Nutrition imeundwa ili kusimamia utekelezaji wa
azma hiyo.”
Waziri
Mkuu amesema kwamba watu wote wanatambua jitihada kubwa zilizowekwa na
Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kupambana na matatizo ya lishe
nchini, ambapo taarifa za wataalamu zinasema kuwa kwa sasa nchi
inakabiliwa na aina mbili za utapiamlo yaani lishe duni na lishe
iliyozidi au iliyokithiri.
Amesema
walengwa wakubwa wa lishe duni ni pamoja na watoto chini ya miaka
mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa hususani wajawazito na
wanaonyonyesha pamoja na vijana balehe (hususan wa kike). “Hii ni kwa
sababu mahitaji ya virutubishi kwa ajili ya miili yao ni makubwa,
ukilinganisha na ule unaohitajika na makundi mengine.”
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments:
Post a Comment