Balozi
mstaafu wa Marekani nchini Tanzania wakati wa utawala wa Serikali ya
awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa, Balozi Charles Stith amesema
anajisikia faraja kusherehekea miaka 20 ya ubalozi nchini kutokana na
mapenzi mema na nchi ya Tanzania.
Balozi Charles amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 20 ya ubalozi ambapo maraisi wastafu mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dk.Jakaya Kikwete walishiriki kwenye sherehe hiyo.
Mbali
ya marais wastaafu, wakati wa sherehe hiyo viongozi wengine wa ngazi
mbalimbali pamoja na wageni waalikwa wakiwemo baadhi ya madaktari bingwa
kutoka Marekani pia walishiriki.
Balozi
Stith alisema akiwa balozi kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2001 amepata
ushirikiano mkubwa kwa Rais mstaafu Mkapa huku Rais mstaafu Dk.Kikwete
wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Amemshukuru
Mkapa na Kikwete kwa ushirikiano ambao walikuwa wakimpatia katika
kuhakikisha uhusiano wa nchi hizo unaendelea na kwamba akiwa nchini
Tanzania amefanikisha kuingiwa kwa makubaliano mbalimbali yenye tija kwa
nchi za Afrika na hasa Tanzania.
“Nimefurahi
kuja Tanzania kukutana na kusheherekea miaka 20 ya Ubalozi.Nimefurahi
kumuona Rais mstaafu Mwinyi,Rais mstaafu Mkapa na Rais mstaafu
Kikwete.Tulishirikiana na tunaendelea kushirikiana,” Alisema Balozi
Stith.
No comments:
Post a Comment