Kamishna na Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi,Paul Chagonja. |
Mkurugenzi
wa Oganaizesheni,Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa CHADEMA,Benson
Kigaila akionyesha barua za maombi ya kufanya maandamano katika maeneo
mbalimbali. (Picha ya Maktaba)
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimedai kufanya maandamano
katika maeneo kadhaa ya nchi na kudai kuwa maandamano hayo yataendelea leo
katika maeneo mengine.
Maandamano hayo yanalengo la kupinga Bunge Maalum la Katiba
linaloendelea mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni ya Mafunzo na Usimamizi wa
Kanda,Benson Kigaila,aliiambia Radio One leo asubuhi kuwa maandamano hayo yamefanyika
katika maeneo ya Songea,Mbinga,Kyela,Chunya,Mbalali,Simiyu,Meatu na Shinyanga.
Akadai kuwa wao wataendelea kuandamana na kwamba si lazima
waombe kibali Polisi, akaongeza kusema wao wanawajibu wa kutoa taarifa Polisi
tu.
Naye Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi,
Paul Chagoja akiongea na Radio hiyo alikanusha na kusema hakuna maandamano
yoyote yaliyofanyika.
Akawasihi wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku na
kutojiingiza kwenye maandamano hayo ambayo alisema si halali.
|
No comments:
Post a Comment