KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 23, 2014

WAZIRI MBARAWA AINGIA MKATABA WA UTENDAJI KAZI NA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YAKE

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof.Makame Mbarawa,akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa utiaji saini mkataba wa Utendaji baina yake na Wenyeviti wa Bodi na Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi zao kwa mwaka wa fedha 2014/14
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote,Prof.John Mkoma, akiweka saini mkataba wa utendaji baina yake na Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mhe.Prof.Makame Mbarawa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi kwa mwaka wa fedha 2014/15
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof.Makame Mbarawa,akipeana mkono na Prof.Mkoma baada ya kuwekeana saini mkataba            

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof.Makame Mbarawa,ameongoza zoezi la utiaji saini Mkataba wa Utendaji baina yake na wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi zao kwa mwaka wa fedha 2014/15.

Lengo la Mhe.Waziri la kuwekeana Mkataba wa Utendaji,na Wenyeviti wa Bodi ni kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu wa Bodi hizo ili kuleta ufanisi na tija kwenye sekta ya TEHAMA , Sayansi na Teknolojia ili iweze kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi na mchango wa sekta kwenye pato la taifa.

Aidha Mhe.Mbarawa alisema mapitio ya utekelezaji wa mkataba huo yatafanyika kila baada ya mizezi mitatu ili kufuatilia namna unavyotekelezwa na kubaini changamoto zinazowakabili wenyeviti na Bodi za taasisi zilizo chini ya Wizara kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha wa 2014/15.

Taasisi zilizo chini ya Wizara ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania,Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia,Kampuni ya Simu Tanzania, Shirika la Posta Tanzania, Taasisi ya Tayansi na Teknolojia,Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya,Taasisi ya sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela,Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.
                                     
                                             

No comments:

Post a Comment