JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
HURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi
la Magereza)
|
TANGAZO
LA NAFASI ZA AJIRA
Jeshi la
Magereza Tanzania Bara linatangaza nafasi za Mafunzo ya Awali ya Askari
Magereza yatakayoendeshwa Chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Mbeya. Waombaji wa
nafasi hizo wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
MASHARTI YA
KUAJIRIWA:
1.
JINSI: Mvulana au Msichana ambaye
hajawahi kuoa
au kuolewa na asiwe na mtoto
2.
URAIA: Awe Raia wa Tanzania Bara
3.
UMRI:
(a)
Wahitimu wa Shahada: Awe
na umri wa kati ya miaka 18 na 28
(b)
Wasio na Shahada: Awe
na umri wa kati ya miaka 18 na 24
4.
UREFU:
(a)
Wavulana: Wawe na urefu
usiopungua Sentimeta 170.2 au Futi
5 na inchi 7
(b)
Wasichana: Wawe na urefu usiopungua Sentimeta
167.64 au
Futi 5 na inchi 4
5.
SIFA
NYINGINEZO:
i)
Awe amehitimu Elimu yake kati ya Mwaka
2012 na 2014
ii)
Awe na Afya nzuri iliyothibitishwa na
Daktari anayetambuliwa na Serikali
iii)
Awe hajawahi kushtakiwa wala
kupatikana kwa kosa lolote la jinai
iv)
Awe na tabia na mwenendo mzuri
v)
Awe hajawahi kuajiriwa mahali popote
Serikalini
7. ELIMU:
(a) Wenye
Shahada katika Fani au Taaluma zifuatazo:
(i)
Shahada ya Sheria (Laws)
(ii)
Utekelezaji wa Sheria (Law Enforcement)
(iii)
Takwimu (Applied Statistics)
(iv)
Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(v)
Mazingira (Environmental Science and
Management or Geography and Environment Studies)
(vi)
Usanifu Majengo (Architecture)
(vii)
Ukadiriaji Majengo (Building Economics)
(viii)
Mipango na Usimamizi Miradi (Project
Planning and Management)
(ix)
Uhandisi wa Umeme (Electrical
Engineering)
(x)
Uhandisi wa Mitambo ya Kilimo (Agricultural
Engineering)
(xi)
Tiba ya Mifugo (Veterinary Medicine)
(xii)
Misitu
(Forestry)
(xiii)
Uchumi Kilimo (Agronomy)
(xiv)
Bima (Insurance)
(xv)
Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika
(Cooperative Management and Accountancy)
(xvi)
(Project Planning and Management)
(xvii)
Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering)
(xviii)
Sayansi ya Kompyuta (Computer Science)
(xix)
Udaktari wa Binadamu (Doctor of
Medicine)
(xx)
Ualimu wa Masomo ya Sayansi kama
Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati
(xxi)
Ualimu wa Masomo ya Biashara na
Kifaransa (Commercial Subjects, Economics and French)
(xxii)
Ukutubi (Library and Information
Studies)
(xxiii)
Mahusiano (Public Relations)
(xxiv)
Biashara na Masoko (Commerce in Marketing)
(b) WASIO NA SHAHADA
1.1:
Wenye Stashahada (Diploma) toka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika
Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i)
Ukutubi (Library)
(ii)
Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(iii)
Bima (Insurance)
(iv)
Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika
(Co-operative Management and Accountancy)
(v)
Mipango na Usimamizi Miradi (Project
Planning and Management)
(vi)
Utabibu (Clinical Medicine)
(vii)
Uuguzi (Nursing)
(viii)
Maabara (Laboratory Technician)
(ix)
Mazoezi ya viungo (Physiotherapy)
(x)
Uandishi wa Habari (Journalism)
(xi)
Ufundi Magari (Automobile Technician)
(xii)
Ujenzi (Civil Engineering)
(ix) Umwagiliaji (Irrigation)
(x) Mitambo ya Kilimo (Agro-Mechanics)
(xi)
Umeme (Electrical Engineering)
(xii)
Usanifu Majengo (Architecture)
(xiii)
Ushauri Nasaha (Counseling and
Guidance)
(xiv)
Uhandisi Mitambo (Mechanical
Engineering)
(xv)
Sanaa na Muziki (Fine and Performing
Arts)
(xvi)
Ualimu wa masomo ya Biashara, Uchumi
na Kifaransa
1.2: Wenye Astashahada/ Cheti cha Majaribio ya
Ufundi katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i)
Uhandisi Maji (Water Engineering)
(ii)
Ujenzi (Masonry)
(iii)
Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)
(iv)
Umeme wa Magari (Auto-Electrical
Engineering)
(v)
Waunganishaji Nondo (Steel Fixing)
(vi)
Useremala (Carpentry and Joinery)
(vii)
Bomba (Plumbing and Pipe Fitting)
(viii)
Rangi (Spray and Painting)
(ix)
Ushonaji (Tailoring)
(x)
Utengenezaji Sabuni (Soap Making)
(xi)
Ufumaji (Embroidery)
(xii)
Kutengeneza viatu (Shoe-Making)
(xiii)
Maabara (Laboratory Technician)
(xiv)
Uhitasi (Secretarial Studies with
Computer Knowledge)
(xv)
Muziki na Utamaduni (Performing Arts and
Music)
(xvi)
Uuguzi na Ukunga (Nursing and Midwife)
(xvii) Utabibu
Usaidizi (Clinical Assistant)
ZINGATIO:
Waombaji wa
nafasi hizi wahakikishe wanazingatia masharti yote yaliyotajwa hapo juu. Upungufu
au udanganyifu wowote utakaojitokeza kwa kutotimiza masharti yaliyotajwa hapo
juu utasababisha maombi kutopokelewa na ikigundulika baada ya ajira mhusika
atasitishwa mafunzo, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani.
8. NAMNA
YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji
wote watume maombi yao moja kwa moja kwa:-
KAMISHNA
JENERALI WA MAGEREZA,
MAKAO MAKUU YA
JESHI LA MAGEREZA,
S.L.P 9190,
DAR
ES SALAAM.
a) Barua
zote za maombi ziambatane na nakala za vyeti vyote vya elimu, ujuzi, Cheti cha
kuzaliwa mwombaji na picha ndogo ya hivi karibuni ya mwombaji (Passport size
photograph). Vyeti halisi na halali vitatakiwa kuoneshwa wakati wa usaili. Hati
za matokeo ya mitihani (Results Slip/ Statement) hazitakubaliwa isipokuwa kwa
wahitimu ambao vyeti vyao halisi havijatolewa na Vyuo husika pekee.
b) Watakaofanikiwa
kuitwa kwenye usaili watajulishwa kupitia katika Tovuti ya Jeshi la Magereza (www.magereza.go.tz), Magazeti na katika Mbao
za matangazo zilizopo kwenye Ofizi za Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Bwalo Kuu
la Maafisa wa Magereza lililopo Ukonga Dar es salaam.
c) Mwisho
wa kupokea maombi ni tarehe 15 Oktoba, 2014.
J. C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
19 SEPTEMBA, 2014
No comments:
Post a Comment