
Mhandisi Happiness Magalula, Naibu Katibu Mtendaji, anayesimamia Klasta
ya Miundombinu na Huduma (mwenye sweta la blue), akitaka ufafanuzi wa
miundombinu ya kuwezesha maji kuwafikia wananchi kutoka katika chanzo
hicho.
Na Mwandishi wetu, Katavi
Bomba la inchi kumi limetandazwa kutoka kwenye chanzo hicho mpaka
mjini ambako kuna tanki kubwa la maji yanayosambazwa katika mji wa
Mpanda na vitongoji vyake
Chanzo cha maji cha chemichemi ya
Ikorongo ambacho ni cha asili kipo kilometa 13.2 kutoka Mpanda Mjini, Mkoani Katavi.
Chanzo hiki cha maji kinazungukwa na miti na uoto wa
asili unaolinda maji hayo yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Katavi,
Magdalena Mkeremi, anasema chanzo hiki cha maji ni chemichemi yenye maji
masafi yasiyokauka hata wakati wa kiangazi.
Chanzo hiki kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni sita kwa siku.
Mradi wa maji wa Mji wa Mpanda ni
wa gharama nafuu kwa sababu hautumii pampu ya aina yoyote, bali maji
husambazwa kwa njia ya mserereko (gravity).
Vile vile maji kutoka kwenye tanki hilo na
kwenda mjini na katika mitaa au vijiji pia hutumia mserereko, hivyo
kurahisisha gharama zake.
Mradi huo wa maji wa vijiji kumi
au mitaa kumi ya mji wa Mpanda unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia chini ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa.
“Maji yalikuwa tatizo kubwa hapa
kwetu lakini ujio wa mradi huu umerahisisha upatikanaji wa maji mjini na
kwenye mitaa ya mji wa Mpanda,” anasema Mhandisi.
Tayari vimejengwa vituo vya
kuchotea maji 41 katika mitaa kumi na watu binafsi wapatao 300
wameunganishiwa maji kupitia chanzo hicho cha maji.
Amesema mradi huo umetekelezwa kwa muda wa miaka mitatu tangu 2012/13 -2014/15 ambapo umekamilika mwezi Septemba 2014.
Amesema ili kuufanya mradi huo
kuwa endelevu wamejenga nyumba ya mlinzi ili kulinda chanzo hicho cha
maji kisiharibiwe kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kulinda
mazingira yanayozunguka eneo hilo.


No comments:
Post a Comment