KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 27, 2014

JITIHADA ZA PAMOJA, KIGEZO CHA KUONDOA MAGONJWA YISIYO AMBUKIZA

Dr Rajagopal & Dr Sanjay Maitra 2
Kushoto ni mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa mkojo na uzazi, Dk.Rajagopal, na upande wa kulia ni mtaalamu wa magonjwa ya figo, Dk. Sanjay Maitra, walipokuja kuona na kutoa tiba kwa wagonjwa  katika kliniki iliyofanyika hosipital ya  Hindu Mandal.

Kuishi ni jambo moja. Kuishi maisha yenye afya njema ni kitu kingine kabisa. Hakuna anaeweza kushuhudia juu ya ukweli huu zaidi ya wale wapatao adha itokanayo na  athari za magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Idadi kubwa ya watanzania  watu wazima na watoto wasio na hatia  ndio waathirika  wanaopata mateso makubwa  kutokana na  aina mbalimbali ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo, ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya figo, mifumo ya neva, uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayohusiana na haya. 

Kwa bahati mbaya, licha ya mipango mikakati ya kupambana na Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa nchini Tanzania, watanzania wengi bado wanaathirika na kufa kupitia magonjwa haya.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya vifo vitokanavyo na magonjwa ya figo nchini Tanzania imefikia 4533 sawa na asilimia 1.03  ya vifo vyote kwa jumla, wakati kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa figo katika Tanzania imeripotiwa kuwa katika asilimia 14 . 

Sababu kuu ya vifo kwa  wagonjwa hawa ni kushindwa kwa figo na mishipa ya  moyo au madhara yatokanayo na matatizo hayo. 

Kujenga mipango endelevu  ya matibabu kwa wagonjwa wa figo, moyo, kisukari, mfumo wa mkojo, mfumo wa neva na uti wa mgongo  inaendelea kuwa changamoto nchini Tanzania.

Shirika la Afya Duniani linapendekeza kwamba, nchi zote zinatakiwa kuwa na  mtaalamu wa mfumo wa neva na uti wa mgongo (neurosurgeon) mmoja kwa kila wakazi 100,000. Hii ni tofauti nchini Tanzania kwani uwiano ni 1: 13,000,000.

No comments:

Post a Comment