KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 30, 2014

DEREVA WA TEKSI ALIYEJIENDELEZA KIELIMU NA SASA AMEKWENDA INDIA KUSOMEA SHAHADA YA UZAMIVU (PHD)

 photo


KIGALI. Juzi Jean Bosco Rusagara aliondoka kwenda Chuo Kikuu cha  Mangalore cha nchini India kwa ajili ya masomo ya Uzamivu katika Uongozi wa Biashara baada ya kupata ufadhili kutoka Baraza la Utamaduni na Uhusiano la India  (ICCR). 

Sasa, wengi wengi watajiuliza kwamba habari ni ipi hapo mtu kupata shahada hiyo ndiyo habari? 

Kinachoifanya hii kuwa ni habari ni kiu ya Rusagara ya kutaka kupata maarifa, hiki ndicho kinachovutia zaidi.

Historia ya Rusagara kielimu

Rusagara, 47, alizaliwa kwenye familia ya hali ya chini ambayo isingeweza kukidhi mahitaji yake ya kielimu, hakuweza kwenda moja kwa moja Chuo Kikuu kupata elimu kwani alikatisha masomo yake akiwa 'O’ level. 

Hata hiyo katika jitihada zake za kupata elimu,aliamua kujifunza udereva . Mwaka 1989 aliamua kutafuta leseni wakati hana gari na baadhi ya marafiki zake walikuwa wakimcheka na yeye aliwaambia msicheke kwani siku moja nitakuja kumiliki ya kwangu.
Baadaye alijiunga na shule ya Sekondari ya Lycée Notre-Dame-d’Espérance iliyoko  Gikondo kwa masomo ya Kidato cha tano na sita.
Baadaye alipata kazi ya udereva kwenya taasisi ya Afya Kigali ambapo alidunduliza pesa yake ya mshahara na hatimaye alinunua gari lake dogo alilolifanya kuwa taksi.

Gari hilo aliliendesha baada ya saa za kazi na kujipatia fedha ambayo ilisaidia kujiunga na Chuo Kikuu cha Kikuu Huria Cha Kigali.
 Kigali. “Nilianza kusoma shahada ya kwanza katika Uongozi wa Biashara 2007 na alihitimu mwaka 2011 baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha kabale kwa masomo ya Shahada ya Uzamili.

KWA HISANI YA NEW TIMES 

No comments:

Post a Comment